Waziri
Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni
ya Msama Promotion Bw. Alex Msama Baada ya kuwasili kwenye uwanja wa
Sokoine tayari kwa tamasha la Krismas lililofanyika kwenye uwanja wa huo
jijini Mbeya , Mh. Fredrick Sumaye amewaasa watanzania kumcha mungu na
kuchagua viongozi waadilifu wenye uzalendo wa nchi, wenye kupenda na
kuhurumia wananchi masikini na wenye hofu ya mungu ili kulinda amani ya
nchi yetu jambo litakalofanya hata maombi yanayofanyika kuombea taifa
la Tanzania yapokelewa na Mungu , Tamasha hilo kesho linaendelea mkoani
Iringa ambapo wakazi wa mjini Iringa wanapata nafasi nyingine ya kumcha
mungu kwa njia ya uimbaji Waziri
Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akisalimiana Katibu wa Baraza la
Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), David Mwasota kushoto ni
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw Alex Msama Waziri
Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akizindua albam ya Kwaya ya Umoja wa
Kwaya ya makanisa mbalimbali jijini Mbeya yenye inayoitwa Mubhopege Pa
Finganilo yenye nyimbo nane kulia ni Katibu wa Baraza la Makanisa ya
Kipentekoste Tanzania (CPCT), David Mwasota na kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw Alex Msama. Katibu
wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), Askofu David
Mwasota akiiombea albam ya Mubhopege Pa Finganilo ya Kwaya ya Umoja wa
Kwaya ya makanisa mbalimbali jijini Mbeya huku Waziri Mkuu mstaafu Mh.
Fredrick Sumaye,Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw Alex Msama
na mmoja wa waratibu wa tamasha la Krismas Bw. John Melele wakishiriki
katika maombi hayo. Mwimbaji
wa muziki wa injili Upendo Nkone akifanya vitu vyake kwenye uwanja wa
Sokoine jijini Mbeya wakati wa tamasha la Krismas leo. Mwimbaji Ambwene Mwasongwe naye amesifu na kuabudu pamoja na mashabiki wake kama anavyoonekana akiwa jukwaani. Mwimbaji
Ambwene Mwasongwe naye amesifu na kuabudu pamoja na mashabiki wake kama
anavyoonekana akiwa akitunzwa na mashabiki wake wakati akiimba
jukwaani. Tumaini Njole na wacheza shoo wake wakiwa angani wakati wakifanya vitu vyao jukwaani. Mashabiki walishindwa kukaa chini wakati wote wa tamasha. Mwimbaji Joshua Mlelwa akikonga nyoyo za mashabiki wake kwa uchezaji wake jukwaani. Mwimbaji Joshua Mlelwa akikonga nyoyo za mashabiki wake kwa uchezaji wake jukwaani. Mashabiki wakipata taswira kwa simu zao huku burudani ikiendelea. Mwimbaji Emmanuel Mgogo naye amefanya mambo makubwa sana katika tamasha hilo. Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akizungumza na mashabiki wa muziki wa injili. Mwimbaji Joshua Mlelwa
akikonga nyoyo za mashabiki wake kwa uchezaji wake na wacheza shoo
wake huyu amekuwa pia akifanya maonesho kama haya Ulaya na Marekani ..
Edson Mwasabwite kulia ni Faraja Ntaboba kutoka DRC Congo wakionyesha vitu vikubwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Mwimbaji
kutoka Kenya Ritha Kisava ambaye ameshiriki Tamasha la Krismas kwa mara
ya kwanza akiimba hii ilikuwa kama utabulisho wake kwa mashabiki wa
muziki wa Injili nchini Tanzania. Waziri
Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akiteta jambo na mmoja wa waratibu wa
tamasha la Krismas Bw. John Melele wakati wa tamasha hilo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MBEYA)