Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015. Pamoja naye ni Mama Salma Kikwete, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe, Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Hamad Msauni na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe Mhe Begum Taj.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wafanyakazi wa ubalozi baada ya kufungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015. Pamoja naye ni Mama Salma Kikwete, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe, Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Hamad Msauni na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe Mhe Begum Taj.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na balozi wa New Zealand nchini Ufaransa baada ya kufungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe Begum Taj. New Zealand ndiyo iliyoiuzia Tanzania majengo hayo ambayo ni ya ghorofa tano ya ofisi pamoja na jengo lingine la makazi ya balozi na maafisa wa ubalozi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mwakilishi wa ubalozi wa Uganda nchini Uraransa baada ya kufungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015. Katikati Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe Begum Taj. Ubalozi wa Tanzania ulikuwa katika majengo ya ubaloizi wa Uganda kabla ya New Zealand kuiuizia anzania majengo hayo ambayo ya ghorofa tano ya ofisi pamoja na jengo lingine la makazi ya balozi na maafisa wa ubalozi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha wageni baada ya kufungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015. 


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua na kuweka saini kitabu cha wageni baada ya kufungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015. Katikati Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe Begum Taj. New Zealand ndiyo iliyoiuzia Tanzania majengo hayo ambayo ya ghorofa tano ya ofisi pamoja na jengo lingine la makazi ya balozi na maafisa wa ubalozi.



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijichanganya na wageni waalikwa ambao ni mabalozi wa nchi mba,limbali za Afrika pamoja na wana Jumuiya ya Watanzania baada ya kufungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015. Katikati Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe Begum Taj. New Zealand ndiyo iliyoiuzia Tanzania majengo hayo ambayo ya ghorofa tano ya ofisi pamoja na jengo lingine la makazi ya balozi na maafisa wa ubalozi. PICHA NA IKULU

photo , ,

 Makamu wa Rais wa Isaca Tanzania Chapter ambaye pia ni Ofisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Serikali Mtandao, Dk. Jabir Bakari akitoa hotuba yake wakati akifungu semina kuhusu usalama wa mifumo ya kompyuta pamoja na ukaguzi wa mifumo hiyo kwa kuwakutanisha wataalumu na kujadiliana kuhusu ukuaji wa teknolojia na usalama.
Aidha Dk. Jabir alisema kuwa semina hiyo inawakutanisha wataalamu wa mifumo ya kompyuta kutoka ndani na nje ya nchi watakaojifunza na kuongeza utaalamu wa kulinda mifumo ya mitandao. 
Naye Mratibu wa Semina hiyo ambaye pia ni Rais wa Isaca Tanzania, alisema kuwa semina hiyo kwa ajili ya kuelezea wadau wa mitandao kuhusu mwelekeo wa teknolojia duniani na ukubwa wa tatizo katika wizi wa mitandao  'miaka ya nyuma kulikuwa na wizi wa kuvunja katika mabenki lakini siku hizi mbinu za wizi zimebadilika na wezi wanaiba kupitia mifumo ua mitandano hasa kompyuta pamoja na simu, kutoa elimu ya ajili ya mifumo ya kompyuta namna ya kuilinda na kuiendeleza.
Katibu wa Tanzania Chapter, Nemayani Kaduma (kulia)akiwa katika semina hiyo.
Baadhi ya washiriki wa semina ya ya kimataifa kuhusu usalama wa mitandao wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Taasisi ya Isaca Tanzania Chapter, Dk. Jabiri Bakari (hayupo pichani) iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Washiri wa semina wakifuatikilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa.
Washiriki wa semina hiyo.
Washiriki.

George Wahome kutoka Isaca-Kenya akitoa mada kuhusu usalama wa mitandao.
Washiriki wa semina.
Rais wa Isaca Tanzania Chapter, Boniface Kanemba akifuatilia mada katika semina hiyo.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Dun & Bradstreet Credit Bureau Tanzania, Adebowale Atobatele akitoa mada katika semina hiyo.
Rais wa Isaca Tanzania Chapter, Boniface Kanemba akizungumza na waandishi wa habari.
Washiri wa semina hiyo wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa.
Rais wa Isaca Tanzania Chapter, Boniface Kanemba (kulia) akimpongeza Isack Maheri  aliyefaulu mitihani ya ukaguzi wa Mitandao ijulikanayo kama CISA.
Rais wa Isaca Tanzania Chapter, Boniface Kanemba (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Isaca Tanzania, Dk. Jabir Bakari (wa tatu kushoto), Katibu wa Tanzania Chapter, Nemayani Kaduma (kushoto) na Mkurugenzi wa Elimu Mtandao, Dk. Carina Wangwe (kulia) na Peter Baziwe (wa tatu kulia)

photo ,

MKATABA wa kujenga tena umoja na kukiunganisha upya Chama Tawala cha Sudan Kusini cha Sudan People’s Liberation Movement (SPLM) ulitiwa saini usiku wa jana, Jumatano, Januari 21, 2015, katika sherehe ya kufana iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Ngurdoto, Wilaya ya Arumeru, Mkoa wa Arusha.
Mkataba huo unaojulikana kama Agreement on the Re-unification of Sudan People’s Liberation Movement umepongezwa kuwa ni hatua muhimu katika kulitoa taifa changa la Sudan Kusini katika hali ya machafuko, vita vya wenyewe kwa wenyewe, kutoelewana na kutoaminiana, mambo ambayo yameligubika taifa hilo tokea mwishoni mwa 2013 wakati kutokuelewana kulipozuka ndani ya SPLM na hatimaye katika Serikali ya nchi hiyo.
Viongozi waliotia saini ni Mheshimiwa Salva Kiir Mayardit, Rais wa Sudan Kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa SPLM na anayeongoza kundi linalojulikana kama SPLM in Government (SPLM-IG), Mheshimiwa Dkt. Riek Machar ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa SPLM na pia aliyekuwa Makamu wa Rais wa Sudan Kusini anayeongoza kundi la SPLM in Opposition (SPLM-IO) na Dkt. Deng Alor Kuol ambaye anaongoza kundi la SPLM Leaders- Former Detainees (SPLM Leaders – FD).
Sherehe hiyo ilishuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho ndicho kimesimamia mazungumzo yaliyozaa Mkataba huo. Rais Kikwete pia ndiye mdhamini mkuu wa Mkataba huo.
Wengine walioshuhudia tukio hilo muhimu ni Rais wa Uganda, Mheshimiwa Jenerali Yoweri Kaguta Museveni; Rais Uhuru Muigai Kenyatta wa Kenya; Naibu wa Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa, Makamu Mwenyekiti wa zamani wa CCM Mheshimiwa John Samwel Malecela ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti wa mazungumzo yaliyozaa Mkataba huo na Katibu Mkuu wa CCM Mheshimiwa Abdulrahman Kinana ambaye alikuwa mwezeshaji wa mazungumzo.
Mazungumzo yaliyozaa Mkataba huo yalianza mwishoni mwa mwaka jana baada ya Rais Kikwete na Chama cha CCM kuombwa na Rais Kiir Mayardit kukubali chama hicho tawala cha Tanzania kutumia uzoefu na ujuzi wake wa miaka mingi wa uongozi na siasa kujaribu kuleta suluhu ndani ya SPLM.
Mazungumzo hayo ya kutafuta suluhu ambayo yamefanyika kwa awamu mbili, ya kwanza yakiwa yamefanyika Oktoba mwaka jana na pili yakiwa yameanza mwanzoni mwa mwezi huu, Januari 2015,  yameongeza thamani kwenye mazungumzo mengine yanayofanyika Addis Ababa, Ethiopia chini ya usimamizi wa taasisi ya IGAD na yanayojadili jinsi ya kurejesha amani nchini humo.
Viongozi wa SPLM wanaamini kuwa kwa sababu mgogoro wa kisiasa nchini mwao ulianzia ndani ya chama hicho na kwa sababu SPLM ndicho chombo pekee ambacho kinawaunganisha wananchi wote wa Sudan Kusini, basi busara inaelekeza kuwa suluhu ianze kutafutwa ndani ya chama hicho.
Mkataba wa jana, kimsingi, unalenga kuweka mazingira ya kujenga utulivu, maelewano, amani na umoja wa kudumu ndani ya chama hicho na nchini humo kwa kuhakikisha kuwa utekelezaji wa mambo ya msingi yaliyokubaliwa kuhusu shughuli za siasa, uongozi na oganisheni ya chama hicho yanafanyika bila kukawia.
Mkataba huo pia unalenga kuhakikisha kuwa chama cha SPLM kinabuni na kutekeleza sera za kuondokana na ukabila, makundi yenye mitazamo finyu na mwenendo wa kijeshi katika siasa za Sudan Kusini.
Aidha, Mkataba huo unalenga kuhakikisha kuwa chama cha SPLM kinafanya mageuzi ya kuanza kujenga utamaduni wa kuvumiliana na ujenzi wa misingi ya demokrasia.
Mkataba huo pia unataka watu wote ambao walishiriki katika mauaji na umwagaji damu katika vita vya wenyewe kwa wenyewe wasiruhusiwe kugombea wala kushika nafasi ya uongozi wa umma ndani ya chama hicho.
Pia viongozi wote wa Sudan Kusini wanatakiwa, chini ya Mkataba huo, kuwaomba radhi wananchi wa nchi hiyo ya Sudan Kusini kwa kuruhusu nchi hiyo kuingia katika machafuko ya umwagaji damu mkubwa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
22 Januari,2015

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe akikaribisha viongozi na wajumbe katika mkutano huo
 Waziri Mkuu Mstaafu na Makamu Mwenyekiti wa zamani wa CCM Mheshimiwa John Samwel Malecela ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti wa mazungumzo yaliyozaa Mkataba huo akisoma muhtasari wa mazungumzo hayo

 Sehemu ya ukumbi wa mkutano huo

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza utiaji wa saini wa  Mhe. Salva Kiir Mayardit  Rais wa Sudan Kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa SPLM na anayeongoza kundi linalojulikana kama SPLM in Government (SPLM-IG), Mheshimiwa Dkt. Riek Machar ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa SPLM na pia aliyekuwa Makamu wa Rais wa Sudan Kusini anayeongoza kundi la SPLM in Opposition (SPLM-IO) na Dkt. Deng Alor Kuol ambaye anaongoza kundi la SPLM Leaders- Former Detainees (SPLM Leaders – FD). 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto), Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) na Bw. Deng Alor Kuol wakionesha hati baada ya kutia saini mkatana wa  makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pongezi kwa Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto), Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) na Bw. Deng Alor Kuol

baada ya kutia saini mkatana wa  makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia wakati  Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) wakipeana mikono na

kubadilishana nyaraka baada ya kutia saini mkatana wa  makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia wakati  Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) wakipeana mikono na

kubadilishana nyaraka baada ya kutia saini mkatana wa  makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.

photo ,


 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua pazia kuzindua nyumba za kisasa za makazi ya wanajeshi akisaidiana na Balozi wa China nchini Mhe Lu Youqing, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga taifa Dkt Hussein Mwinyi na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange Gongo la Mboto jijini Dar es salaam.
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia kwa pamoja na baadhi ya viongozi baada ya kuzindua nyumba za kisasa za makazi ya wanajeshi akisaidiana na Balozi wa China nchini Mhe Lu Youqing, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga taifa Dkt Hussein Mwinyi na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange Gongo la Mboto jijini Dar es salaam.
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili tayari kuzindua nyumba za kisasa za makazi ya wanajeshi Gongo la Mboto jijini Dar es salaam. 
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa mradi huo wa nyumba za kisasa za makazi ya wanajeshi Gongo la Mboto jijini Dar es salaam.
  Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa mradi huo wa nyumba za kisasa za makazi ya wanajeshi Gongo la Mboto jijini Dar es salaam.
  Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa mradi huo wa nyumba za kisasa za makazi ya wanajeshi Gongo la Mboto jijini Dar es salaam.

Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wanajeshi baada ya kuzindua  nyumba za kisasa za makazi ya wanajeshi Gongo la Mboto jijini Dar es salaam. PICHA NA IKULU

photo , ,


Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Kwenye Ofisi ya Mtendaji  kata ya Mlimani Katika Mfululizo wa Ziara zake katika Kata mbalimbali Jimbo la Morogoro mjini.

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akikagua Vifuko vya mndihira na Mwere Vilivyo Kata ya mlimani Ambavyo Vimegarimu Kiasi cha Shilingi Milion 3 Zilizotolewa na Mbunge Huyo.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akianda Safu ya Milima Uluguru Kuelekea Mitaa ya Kisosa ,Choma na Chalagule vilivyopo Kata ya Mlimani 
 
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akisikiliza kwa Makini Kero Mbalimbali zilizokuwa Zikiwasilishwa na wakazi wa Kata ya Mlimani Jimbo la Morogoro Mjini wakati Mbunge huyo aliopofanya ziara ya Kutembelea kata Hiyo.
Baadhi ya Wakazi wa Mitaa ya Ruvuma ,Mng'ong'o, na Tulo Iliyopo Kata ya Mlimani Wakimsikiliza kwa Makini Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini alipofanya ziara katika Mitaa hiyo ili kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wakazi wa Kata hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akisisitiza Jambo wakati Akiongea na wakazi wa Kata ya Mlimani
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akijibu Hoja Mbalimbali Mara baada ya  Kusikiliza Kero zinazowakabili wakati wa Kata  ya Mlimani  Ambapo walimwambia Wanakabiliwa na Kero Kubwa ya Umeme,Maji na Barabara.Kuhusu Maji Mh Abood alitoa Zaidi ya Shilingi Shilingi Milioni 20 Kwajili ya Kununua Vifaa vya Kuwezesha Kufikisha Maji katika Mitaa ya Kisosa ,Choma , Chalagule Ruvuma Mng'ong'o na Tulo Iliyopo Kata ya Mlimani. .Pia Alitoa vifaa vyenye Dhamani ya Shilingi Milion 2 kwajili  ya Kununua Vifaa vya Kukarabati Barabara  Za Mitaa hiyo Ikiwemo Sajuri,Makaravati na Vifaa vingine vinavyotumika kutengeneza Barabara.
  Wakazi waliojitokeza kwenye ziara ya Mbunge huyo
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akipokea zawadi Kutoka kwa Wakazi wa Mitaa ya Kisosa ,Choma na Chalagule  Ikiwa ni Ishara ya kukubali Utendaji wa Kazi wa Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini.Wakielezea Zaidi wakazi hao wamesema Tangu Uhuru hakuna Mbunge aliyewahi kuwatembelea na pili Ahadi zote alizowahidi wakati wa Mitaa hiyo amezitekeleza na bado wana imani kubwa sana na Mbunge Huyo.Namnukuu Mkazi Mmoja aliyejitambuliza kwa Jina la Bw Omari Alisema " Huyu Ndiye Mbunge tunayemuhitaji Mbunge wa Vitendo na si Mbunge wa Maneno Mengi Utendaji Hafifu"
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akiwa na mtendaji wa kata ya Mlimani mara baada ya kuwasili katika Mitaa ya Ruvuma Mng'ong'o na Tulo Iliyopo Kata ya Mlimani.
Wajumbe wa Serikali ya mtaa wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood 
Wakazi wa Mtaa wa Kikundi wakiwa Kwenye  Mvua Kumsikiliza Mbunge wao

photo , ,