Mbunge
wa bunge la Afrika Mashariki (EALA), kutoka Tanzania, Mh.Abdullah
Mwinyi, (katikati-wapili kulia), akipewa maelezo na meneja wa soko la
samaki Ferry, Bw.Solomon Mushi, kuhusu biashara ya samaki sokoni hapo
leo Aprili 20, 2016.
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
WABUNGE
wa bunge la Afrika Mashariki, (EALA), kutoka Tanzania, wameendelea na
ziara za kutembelea shughuli za kiuchumi za wananchi na leo Aprili 20,
2016 walikuwa kwenye soko la samaki la kimataifa ferry jijini Dar es
Salaam.
Wabunge
hao wakongozwa na mwenyekiti wao, Mh. Makongoro Nyerere, Wamewaeleza
viongozi wa wavuvi, wakaanga samaki na wapaa samaki fursa zilizopo
kwenye ushirikiano wa Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki ambapo kwa
sasa lina jumla ya nchi wanachama sita, Sudan Kusini ikiwa ndio
mwanachama wa hivi karibuni kabisa.
Wabunge
hao pia wametembelea na kujionea shughuli zihusianazo na samaki kwenye
soko hilo. Pia walipata fursa ya kusikiliza maoni mbalimbali ya wadau
hao katika soko la samaki Ferry. Soko lasamaki Ferry ni moja ya maeneo
yanayotoa ajira kwa vijana wengi hapa jijini Dar es Salaam, ambao
ukiacha wavuvi wao hufanya kazi ya kupaa samaki, kushusha samaki kutoka
kwenye mitumbwi na kukaanga samaki. Pia kuna akina mama na baba wanaotoa
huduma za chakula.
Mh.
Mwinyi, akizungumza wakati wa kikao cha kubadilishana mawazo baina ya
wabunge hao nawashika dau kwenye soko hilo, wengine kutoka kushoto ni
Meneja wa soko hilo, Bw. Mushi, Mwenyekiti wa bodi ya soko ambaye pia ni
diwani wa kata ya Kivukoni jijini Dar es Salaam, Mh.Masaba, Mwenyekiti
wa wabunge wa EALA-Tanzania, Mh. Makongoro Nyerere, na Mh. Nderaikindo
Kessy
Mvuvi akieleza maoni yake mbele ya wabunge hao.
Shughuli za samaki zikiendelea kwenye moja ya mabanda ya soko hilo.
Mh.
Makongoro Nyerere (kulia), akizungumza. Kushoto niMwenyekiti wa Bodi ya
soko ambaye pia ni diwani wa Kata ya Kivukoni, Mh. Masaba.
Kijana akiwa amebeba samaki wakubwa baada ya kuwatoa magamba
Kijana akiwa amebeba samaki kuelekea mahala pa kutolea magamba
Mh. Mwinyi akipeana mikono na meneja wa soko hilo, Bw. Mushi
0 Responses so far.
Post a Comment