Tumo katika taifa lililogubikwa na maswali. Watu hawaoni tena nuru kwa maisha yao ya baadae. Mazungumzo ya watu barabarani, kwenye vyombo vya usafiri, vyombo vya habari, maofisini, sehemu za ibada, vijiweni na kwenye mikusanyiko ya watu hujiuliza tunakwenda wapi. Ugumu wa maisha umewafanya wengine wazikimbie familia zao huku wengine kwa kuchanganyikiwa wamejiua na kuua familia zao.


Hali ya kukata tamaa iliyoenea miongoni mwa wananchi wengi haitokani tu na matatizo peke yake wala maovu katika jamii. Kinachokatisha tamaa zaidi ni kuona viongozi walioapa kuwalinda wanananchi dhidi ya uovu wakicheka na uovu wenyewe na wakati mwingine wanakumbatiana na waovu hadharani. Mpaka sasa hakuna dalili kwa viongozi kumaliza kucheka 


Serikali sasa inakabiliwa na changamoto nyingi kutoka kila upande. Ni kama mfumo mzima wa utawala umesimama na Mungu ndiye ajuaye nini kitatokea kesho na keshokutwa ndani ya taifa letu.  Nchi inakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira, umasikini uliokithiri, rushwa hususan kwenye mikataba ya kinyonyaji inayowanufaisha watu wachache katikati ya mamilioni ya watanzania. Uporaji wa rasilimali za taifa, mishahara midogo isiyoendana na hali ya maisha, kuporomoka kwa uchumi na huduma mbovu za kijamii ni baadhi tu ya dalili za ugonjwa hatari uliolikumba taifa.

(Hayo ni moja ya maelezo yaliyomo ndani ya kitabu changu cha shukrani ninachotarajia kukizinduwa mwishoni mwa mwezi wa tatu, kwa watakaohitaji nakala ya kitabu wasisite kunitafuta kupitia 0787 070707)

photo ,

Moja ya mambo ambayo kijana wa leo anaweza kujivunia ni namna anavyoweza kushiriki kikamilifu katika mambo ya siasa. ni vema tukakumbuka kuwa hata mwasisi wa Taifa hili Mwalimu Julius Nyerere wakati wa harakati za kudai uhuru yeye pamoja na wapigania uhuru wengi wa afrika walikuwa bado vijana, wenye nguvu na hali ya pekee katika kupigania haki za wanyonge.

Kama vijana hawashiriki kikamilifu katika mambo ya siasa, siku moja watakuja kujikuta wametawaliwa na mtu wa Hovyo, mpumbavu na mwendawazimu, nchi zote zilizo huru duniani viongozi wake huchaguliwa kupitia michakato ya kisiasa, Mwalimu Nyerere aliwahi kusema ili nchi iendelee inahitaji vitu vinne navyo ni ardhi,watu, siasa safi na uongozi bora.

Ni vema tukatambua pia kuwa siasa sio chafu kwa asili yake bali kuna viongozi wachafu ndani ya siasa, hawa ndio wanaoichafua taswira nzuri ya siasa

hivyo basi......Ukiona vijana kama akina Mnyika, Tundu Lisu, Halima Mdee, David Silindi, Kafulila,Joshua Nassari na wengineo wengi wanapigania haki za wanyonge, usipowaunga mkono,ukiwapinnga sasa, nawe ukiwa mzee utapingwa pia

photo

Kuna jambo tunaweza kujifunza kutokana na picha hii

photo


Mwanzoni mwa miaka ya tisini, chama cha mapinduzi kilianzisha mradi mchafu wa kisiasa kilipobaini uwezekano wa kusombwa na kimbunga cha uchaguzi. Kiliogopa kukataliwa na wananchi katika uchaguzi mkuu wa rais na wabunge wa mwaka 1995. Katika kutimiza malengo hayo, chama cha mapinduzi kilitafuta wataalam wa propaganda ili wabuni mradi wa hofu. Wakaeneza uzushi eti vyama vingi husababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe.


Chama cha mapinduzi kikajaza watu hofu ya kupoteza maisha, kukatwa viungo, kupoteza ndugu na jamaa kwa vita iwapo watachagua upinzani. Walitoa sababu nyingi za kutochagua upinzani kwa kuinganisha na mauaji ya Rwanda, Burundi, sudan na Somalia.


Vyombo vya habari, hasa vya elektroniki vikasambaza hofu kwa kuonyesha picha za mauaji ya Rwanda na Burundi vikiwa na lengo la kuhujumu ustawi wa demokrasia na vyama vingi. Na  Kwakuwa wakati vyama vingi vikianzishwa watu wengi hawakuwa na uelewa wa kutosha juu ya mfumo wa siasa za vyama vingi, wengi wakalaani mfumo wa vyama vingi bila kujua kuwa vilianzishwa kikatiba


Walianza kuvuana magamba wenyewe kwa wenyewe wakasahau kuwa Kuvuana magamba kwa sasa ni sawa na kitendo cha kuweka maua mazuri juu ya kaburi la zamani. Maua hayo hayasaidii chochote kwa marehemu zaidi ya kufurahisha macho ya watu wengine wanaolitazama kaburi kwa nje.

Kwa wale watakaokumbuka, wakati ule chama cha wananchi CUF kilipokuwa ni chama kikuu cha Upinzani CCM walipandikiza chuki kwa propaganda kuwa CUF ni chama cha waislam hivyo kwa kiasi kikubwa wakafanikiwa kuigawa CUF na wakristo. Miaka michache baadae Chama Cha Demokrasia na maendeleo baada ya kuonekana kukubalika sana miongoni mwa watanzania CCM wakaja na propaganda ile ile waliyoitumia kwa CUF kwa kuiunganisha CHADEMA na ukristo na ukabila, ingawa propaganda hii haijawa na mashiko miongoni mwa watanzania wa leo lakini wapo baadhi ya watu ambao bado hawaelewi kama huo ni mchezo mchafu wa CCM................
(Maelezo haya yameelezwa kwa kirefu ndani ya kitabu changu cha shukrani)
  

photo ,

Mbunge mtarajiwa wa Morogoro mjini kupitia CHADEMA Bw. Amani Theophilus Mwaipaja ,anatarajia kuzindua KITABU chake tarehe 30/03/2013 mjini Morogoro,ambamo ndani yake kitakuwa mahususi kwa ajili ya SHUKRANI kwa wapenda maendeleo wote na wanaharati wote wa ukombozi wa wanyonge na  pia waliokuwa nae bega kwa bega katika uchaguzi uliopita. Katika uzinduzi huo anatarajia kuzindua na blog yake na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Kiongozi wa kitaifa wa CHADEMA. Kama unahitaji KITABU hicho ufanye mawasiliano mapema kwa simu: 0787 070 707 na 0714 559 910.

photo

Kutoka kushoto:Uhuru Kenyatta na William Ruto wakiteta Jambo katika kampeni zao za mwisho za uchaguzi ujao wa Kenya ,utakaofanyika jumatatu tarehe 4/3/2013 ,walitembelea mitaa ya Kapkatet, Bungoma na Homabay nchini Kenya ,wao wakiwakilisha kundi la JUBILEE.
Uhuru Kenyatta(gari la bluu)  na William Ruto (gari jekundu) wakiwa katika magari ya wazi katika kampeni zao za mwisho za uchaguzi ujao wa Kenya ,utakaofanyika jumatatu tarehe 4/3/2013 ,walitembelea mitaa ya Kapkatet, Bungoma na Homabay nchini Kenya ,wao wakiwakilisha kundi la JUBILEE.


Uhuru Kenyatta na William Ruto wakitaka kuyarudi mangoma katika kampeni zao za uchaguzi ujao wa Kenya ,utakaofanyika jumatatu tarehe 4/3/2013 ,walitembelea mitaa ya Kapkatet, Bungoma na Homabay nchini Kenya ,wao wakiwakilisha kundi la JUBILEE.
William Ruto akiteta Jambo katika kampeni za mwisho za uchaguzi ujao wa Kenya ,utakaofanyika jumatatu tarehe 4/3/2013 ,walitembelea mitaa ya Kapkatet, Bungoma na Homabay nchini Kenya ,wao wakiwakilisha kundi la JUBILEE.
Huu ni UMATI wa watu waliokuja kuhudhuria kampeni za JUBILEE katika mitaa ya Kapkatet, Bungoma na Homabay ,uchaguzi utakafanyika jumatatu tarehe 4/3/2013
Mwana dada akifurahia kampeni za upande wa JUBILEE ,akiwa amevaliwa vazi lenye jina la chama cha TNA ambacho Uhuru Kenyatta ndie anakiwania nacho urais wa Kenya Jumatatu Ijayo. Kwa hisani ya Wazalendo 25 Blog

photo


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ujumbe maalumu kutoka kwa Rais Omar El Bashir wa Sudan ulioletwa na Mhe.Dkt.Nafie Ali Nafie ikulu jijini Dar es Salaam  Jana asubuhi.Picha na Freddy Maro-IKULU

photo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maal: umu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia.
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe Ban Ki-moon akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maal: umu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia.
 Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa Dkt  Nkosazana Clarice Dlamini-Zuma akisaini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia.
 Rais Joseph Kabila wa DRC na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakibadilishana mawazo kwa furaha huku Rais wa Jamhuri ya Kongo (Brazaville) Mhe Denis Sassou Nguesso akiwa kati yao baada ya wote kweka saini  katika Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia.
 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe Shamsi Vuai Nahodha pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Mahadhi Juma Maalim na wajumbe wengine wa ujumbe wa Tanzania wakati wa uwekaji akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon kwa kuwa mmoja wa viongozi wa bara la Afrika walio mstari wa mbele kusimamia amani baada uwekaji akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Desalegn baada uwekaji akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa Dkt  Nkosazana Clarice Dlamini-Zuma
Rais wa Rwanda Paul Kagame  akiisaini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe Ban Ki-moon katika picha ya pamoja na viongozi wa nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu baada ya uwekaji akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia,  Februari 24, 2013.Picha na IKULU
---

STATEMENT BY H.E. JAKAYA MRISHO KIKWETE, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA AT THE SIGNING CEREMONY OF THE PEACE, SECURITY AND COOPERATION FRAMEWORK FOR THE DEMOCRATIC REPUBLIC OF CONGO (DRC) AND THE REGION,24TH FEBRUARY 2013, ADDIS ABABA, ETHIOPIA.
-- 
Your Excellency Haillemariam Desalegn, Prime Minister of the Federal Democratic Republic Ethiopia and Chairperson of the African Union;
Excellencies Heads of State and Government;
Your Excellency Ban Ki-moon, Secretary General of the United Nations;
Your Excellency Dr. Nkosazan Dlamin Zuma, Chairperson of the African Union Commission;
Invited Guests;
Ladies and Gentlemen.

This is a very auspicious and historic day for the people of the Democratic Republic of Congo, her neighbours and the entire Great Lakes Region. It is a momentous day for the Southern African Development Community (SADC), Africa, the African Union, United Nations and the entire international community.

  The people of the DRC have suffered for too long. They deserve a break. They deserve to live a better life; a life where their safety and security is assured and guaranteed; a life where they pre-occupy themselves with more important things for improving their living conditions. 

The signatures we have just appended to the Framework is a solemn undertaking and commitment to deliver on the aspirations of the people of DRC and the Great Lakes Region for peace, security, stability and cooperation.

On behalf of the Government and people of the United Republic of Tanzania I promise that we will play our part accordingly.

In conclusion, I commend the Secretary General of the United Nations, H.E. Ban Ki-Moon for this great initiative. I thank the AU Commission Chairperson, H.E. Nkosazana Dlamini Zuma for the Leadership which made this event possible. 

Last but not least, I thank the Prime Minister of Ethiopia and Chairperson of the African Union, H.E. Hailemariam Desalegn for his wise leadership and warm reception and gracious hospitality accorded to us.

I thank you for your kind attention.

photo

Baada ya kimya cha muda mrefu globuni,sasa nimerudi rasmi.



Mh Amina chifupa akiapa mbele ya Bunge.....nimeipenda picha hii, wewe je?

photo ,

Nani alaumiwe kwa hili?



Picha hii nimetumiwa na mdau kutoka jijini Arusha...ni kama anasikia raha eh?


Wanakijiji nikumbusheni...mnyama huyu huwakilisha nnini kwenye hela yetu?
Unaweza kupagundua mahali hapa? hivi watu wa mipango miji wanajua madhara ya kuruhusu ujenzi wa namna hii?ebu wadau wasilisheni hoja maana kila nikikumbuka kile kilichotokea katika soko la mwanjerwa moyo wangu huruka kichurachura



Aliyekuwa Rais wa Benki ya Dunia akitafakari jambo......


Usipomjua huyu wewe si Mtanganyika....anaitwa nani vile?


Wapi hapa?


Hili ndilo kundi la Acappella kutoka Africa ya kusini lijulikanalo kama Ladysmith black Mambazo.Kundi hili linaimba muziki wa asili bila kutumia vyombo vya muziki yaani akapela na lilianzishwa mwaka 1964 na kiongozi wa kundi hilo - wa kwanza kutoka kushoto mstari wa mbele ambaye anaitwa Joseph shabalala.
Kundi hili ni moja ya vikundi maarufu duniani vinavyoimba muziki wa acappella kutoka Africa na kwa taarifa yako limesafiri na kushirikishwa na waimbaji mbalimbali maarufu duniani. Sauti za kundi hili ndizo zinazosikika katika ile picha ya Eddie Murphy iliyotokewa kupendwa sana ya COMING TO AMERICA.kama hujawahi kuitazama nenda kaikandamize sasa hivi.
Jamaa hawa wako mbioni kuja nchini Tanzania kwa udhamini wa Nyanza Company Limited


Hii imekaaje?
Mwanamke wa shoka...unamkumbuka huyu?.....hata kama humkumbuki lakini amini kuwa siku hazigandi


Hii ndiyo njia inayoelekea kituo cha watoto yatima Simike jijini Mbeya.......Kituo cha Simike kimeanzishwa miaka 17 iliyopita, wadau naomba niwapeleke moja kwa moja mkajionee wenyewe mandhari ya huko ili tusaidiane kwa pamoja katika kuwasaidia hawa wadogo zetu.
Safari yangu kuelekea kinjia hiko juu ilianzia hapa


Mtoto huyu umuoneaye hapo alipo hasikii, haoni na wala haongei.
Ni mmoja wa watoto yatima wanaolelewa na kituo cha Simike jiji Mbeya.



Mtoto huyu anayejulikana kwa jina la Amani ni mmoja kati ya watoto yatima wanaolelewa na kituo cha watoto yatima cha Simike...Mtoto huyu alipelekwa kituoni hapo akiwa na umri wa wiki moja baada ya mama yake aliyemzaa kumtelekeza katika hospitali ya wazazi ya Meta.Hapa alikuwa akiwaimbisha wenzake.
Watoto hawa wanahitaji msaada wako, hata kuwatembelea na kuwajulia hali na kuongea nao ni sehemu mojawapo ya kuwapatia faraja


Mazingira ya ndani.....mbele ya hilo pipa kwa upande wa kulia ndipo kilipo chumba hiki hapa chini


Chumba hiki hutumiwa kama sebule na darasa kwa watoto wa kituo cha Yatima Simike


Wema Sepetu? !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Wadau toeni maoni juu ya hili......mimi naona haikubaliki totally


Ni vitu vya kawaida ukiwa ughaibuni kutinga makoti kama haya....nimepozi na Frank Zacharia..Mkurugenzi wa Nyanza Company Limited



Ukiingia tu ndani ya geti la Hospitali ya wazazi Meta karibu na jengo la damu utakaribishwa na ujumbe huu


Wabongo wengi wamekuwa na kasumba ya kuogopa kutoa damu...hivi tatizo ni nini?ukosefu wa elimu au?Michuzi unasemaje?kama huogopi njoo


Afande Sele akiwa katika pozi ndani ya gari lililokuwa likitumiwa na tour ya wanaume halisi na ndege tunduni...jamaa anatisha sana katika utunzi wa mashairi yaliyokwenda shule....Kitururu unamzungumziaje mshikaji huyu?...toa hoja



Hawa ni moja ya wadau wangu wa blog hii ambao nao wanakandamiza digrii ya sheria ughaibuni....jamaa anaitwa Keny ambaye pia ni mtunzi mashuhuri wa mashairi ya kidhungu...huyo mdada aliyenaye ndiye my nanii wake