Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akimpongeza Mkurugenzi wa JAMII KWANZA Bw. Amani Mwaipaja baada ya kuanzisha kampeni ya Jamii Kwanza mjini Morogoro.

Mgeni rasmi Mhe. Bernard Membe akikabidhiwa picha yake iliochorwa kwa mkono na msanii Bw. Chipenya wakati wa uzinduzi wa kampeni ya JAMII KWANZA nadni ya Ukumbi wa Glonency -88 mjini Morogoro.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Lazaro Nyalandu akitoa Mchango wake kwa Kampeni ya  JAMII KWANZA.



Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa na nakala ya kitabu changu cha Zijue Sheria na Haki Zangu

photo ,


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425

PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Eng. Omari Jumanne Bakari kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO).

Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue, uteuzi huo umeanza Desemba 04, mwaka huu, 2013. Eng. Omari Jumanne Bakari ni Mtafiti Mwandamizi katika Tume ya Sayansi na Teknolojia, Dar es Salaam.

Eng. Omari Jumanne Bakari ni Mtanzania mwenye elimu, weledi na uzoefu ambao umemfanya Mheshimiwa Rais aamini kuwa atakapoongoza SIDO, atasaidia kukidhi matarajio ya taifa kwa kueneza ujasiriamali, uwekezaji,uzalishaji na kutoa nafasi za ajira katika ngazi ya viwanda vidogo na vya kati kama msingi imara wa uchumi wa Tanzania, ikiwemo kwa kuingiza sayansi, teknolojia na ubunifu katika viwanda vidogo vidogo.
         “Mwisho”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
DAR ES SALAAM.

16 Desemba, 2013

photo ,


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe George W. Bush na Mkewe Laura Bush wakiwa jukwaa la viongozi na watu mashuhuri baada ya Kuadhimisha Kumbukumbu ya Kifo cha aliyekuwa kiongozi mashuhuri wa Afrika Kusini na duniani, Mheshimiwa Nelson R Mandela leo Desemba 10, 2013 katika uwanja wa FNB jijini Johannesburg.Picha na IKULU
---
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Desemba 10, 2013, ameungana na viongozi wa mataifa mbali mbali duniani na maelfu ya wananchi wa Afrika Kusini Kuadhimisha Kumbukumbu ya Kifo cha aliyekuwa kiongozi mashuhuri wa Afrika Kusini na duniani, Mheshimiwa Nelson R Mandela.

Maelfu kwa maelfu ya wananchi wamehimili mvua kubwa iliyokuwa inanyesha kwa nguvu kwenye Uwanja wa Michezo wa FNB mjini Johannesburg kumwaga Mzee Mandela ambaye alikuwa ishara kuu ya upinzani wa siasa za ubaguzi wa rangi za makaburu wa Afrika Mashariki.

Mheshimiwa Mandela ambaye alifariki duniani Ijumaa iliyopita, Desemba 5, 2013, alikuwa Kamanda wa Jeshi la Ukombozi la Chama cha African National Congress la Umkhoto we Sizwe akafungwa jela kwa uhaini kwa miaka 27 na utawala wa Makaburu.

Baada ya kutoka jela mwaka Februari 1990, Mzee Mandela alichaguliwa kuwa Rais wa Kwanza wa Afrika Kusini ya mwaka 1994. Lakini Mheshimiwa Mandela alitumikia kipindi kimoja tu cha miaka mitano na kukataa kutumikia kipindi cha pili.

Kiasi cha viongozi 91 kutoka sehemu duniani wamehudhuria Kumbukumbu hiyo iliyokuwa na kila aina ya mchanganyiko wa hisia – wengine wakiwa na majonzi na wengine wakicheza na kuimba kwa muda wote wa shughuli hiyo iliyochukua kiasi cha jumla ya saa tano. 

Mbali na Rais Kikwete ambaye amefuatana na Mama Salma Kikwete, marais wengine mashuhuri duniani waliohudhuria Kumbukumbu hiyo ni Mheshimiwa Barack Obama wa Marekani, Mheshimiwa Francois Hollande wa Ufaransa, Waziri Mkuu wa Uingereza, Mheshimiwa David Cameroun na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Ban Ki Moon.

Kumbukumbu hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi wa zamani wa Marekani wakiwemo marais watatu wa zamani wa Marekani – Mheshimiwa Jimmy Carter, Mheshimiwa Bill Clinton na Mheshimiwa George W Bush na mawaziri wakuu wawili wa zamani wa Uingereza, Mheshimiwa Tony Blair na Mheshimiwa Gordon Brown.

Rais Kikwete kesho, Jumatano, Desemba 11, 2013, ataungana na viongozi wenzake katia katika kutoa heshima za mwisho na kuuaga rasmi mwili wa Marehemu Mandela ambao utawekwa kwenye Majengo ya Urais wa Afrika Kusini ya Union Buildings mjini Pretoria.

photo ,

 Wasanii wa Kikundi cha ngoma wakitumbuiza wakati wa Tamasha la mimi ni Afrika,Afrika ni mimi
 Kikundi cha ngoma kikiendelea kutumbuiza


 Mshehereshaji wa Tamasha la mimi ni Afika,Afrika ni mimi Adam mchomvu akiongea na wakazi wa arusha waliojitokeza kwa wingi kwenye viwanja vya general tyre.

 Adam mchomvu akifurahi na wakazi wa arusha
 Wakazi wa Arusha wakinyoosha mikono juu kama ishara ya kupinga rushwa.
 Msaniii chaba akiwaburudisha wakazi wa Arusha
 Msanii chaba na back voclist wake wakiendelea kutawala steji kwenye viwanja vya general tyre
 Nasty Nastyyyy msaniiii chaba akiimbaaaa jukwaaani
 Msanii Joh makini akiwa kwa steji akiwaburudisha wakazi wa Arusha kwenye Tamasha la kupinga Rushwa mimi ni afrika na afrika ni mimi.
 Kundi la weusiiiiii wakikamata steji vilivyo jana kwenye viwanja vya general tyre


 Sema beiiii ya mkaaa,bei ya mkaaaa kundi la weusi wakiwaimbisha wakazi wa arusha kwenye Tamasha la kupinga Rushwa la mimi ni afrika na afrika ni mimi



 Dogo janja akiwa kwa steji akiwarusha mashabiki
 Kundi la jambo Squadwakirukaaa kingarerooooo na mashabiki wao
 Machaliii machaliiiii wa araaaaa hivyo ndio ilikuwa ikisikika wakati jambo squad wakifanya yao jukwaaani.
 Msanii stamina akiwa kwa steji akiwarusha mashabiki

Lile tamasha la kupinga matumizi ya Rushwa na utoaji limefana sana jana Jijini Arusha kwenye viwanja vya general tyre.Kauli mbiu ya tamasha hilo ilikuwa "RUSHWA SIO" na kubebwa na ujumbe mzito wa mimi ni afrika na afrika ni mimi.
Dhumuni kubwa la tamasha hilo ilikuwa ni kutoa elimu kwa wanainchi juu ya madhara ya utoaji na upokeaji rushwa,kiingilio ilikuwa ni bure kabisaaa.Sambamba na elimu iliyotolewa viwanjani hapo pia wakazi wa Jiji la arusha walipata nafasi ya kupata burudani ya kufa mtu kutoka kwa wasanii kama izo b,stamina,weusi,chindo man,roma,fid q,linah,naziz na vanessa mdee.
  PICHA NA HABARI KWA HISANI YA DJ SEK BLOG

photo ,

 Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akipongezwa na Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kwa kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Mbunge, jioni mjini Mbalizi, jijini Mbeya. Viongozi hao wamo kwenye ziara ya kuimarisha chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Akizungumzia uteuzi huo, mjini Mbalizi jioni hii,

Dk. Migiro amemshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa uteuzi huo ambao ameupokea kwa furaha, na kueleza kuwa kitendo hicho kinadhihirisha jinsi Rais Kikwete alivyo na imani naye pamoja na imani kwa Wanawake wa Tanzania
 Dk. Migiro (kulia), akipongezwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwa uteuzi wake huo.
 Dk. Migiro akizungumza na vyombo vya habari, jinsi alivyopokea kwa furaha uteuzi wake huo.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akimpongeza Dk. Migiro kwa kuteuliwa na Rais Kikwete kuwa Mbunge.

photo ,