Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi (Mb), (Mwenye kaunda suti nyeusi) akisalimiana na Makamanda wa JWTZ mara baada ya kupokelewa na Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Luteni Jenerali Samuel Ndomba (Aliyesimama kulia kwa Mhe. Waziri) muda mfupi kabla ya Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye Kikosi cha Komando kuanza ziara yake ya kujionea hali na utimamu wa vikosi vya JWTZ Mkoani Morogoro.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea taarifa ya Utawala na Utendaji kivita kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha Komando wakati wa ziara yake.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipewa maelezo kwa kutumia mchoro kuonesha mzunguko mzima wa maeneo atakayotembelea katika kikosi cha Komando.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia kupitia kilengeo maalum kinachotumiwa kwenye silaha na makomando kulengea shabaha.
Makomando wakimuonesha Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (hayuko pichani) mapigano bila shilaha wakati wa ziara yake.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia mapambano ya kareti, taikondo na judo yaliyokuwa yakioneshwa na makomando wa JWTZ (Hawamo pichani).
Komando wa JWTZ akionesha uwezo wa kukwepa mapigo ya risasi za adui kwa kupita juu ya mapigo hayo kwa kutumia kamba na kisha kuendelea na jukumu alilopewa.
Kamanda wa Kikosi cha Uhandisi wa Medani akitoa taarifa ya Utawala na Utendaji Kivita kwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (Hayupo pichani) mara baada ya Kikosi hicho kutembelewa.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifafanua maeneo kadha ambayo Wahandisi Medani wa JWTZ wamefanya kazi nzuri kurejesha miundombinu ya reli, barabara na madaraja hata pale ambako Mamlaka za Kiraia zimekuwa na maoni kuwa kazi hizo zingehitaji muda mwingi zaidi.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo kuhusu baadhi ya mitambo mipya ya kutengeneza barabara katika Kikosi cha Uhandisi Medani.


Picha/habari na Luteni Kanali Juma Nkangaa Sipe, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ulinzi na JKT

photo ,

0 Responses so far.