Mlima maarufu wa Chamanyani upo katika wilaya ya Morogoro Vijijini. Mlima huu upo njiani kama unaenda vijiji vya Mvuha, Dutumi au Kisaki. Kwa wale walio wahi kupita Mlima Kitonga huufananisha Mlima Chamanyani na Mlima Kitonga kutokana na kuwa na kona nyingi na za hatari. 

Mlima huu ni sehemu ya kivutio  kikubwa kwa wasafiri waendao Morogoro Vijijini. Wenyeji wanadai kuwa Asili ya Jina "Chamanyani" ni kutokana na Mlima huo kuwa na Nyani wengi
Ukarabati wa Miundombinu ukiendelea ndani ya Wilaya ya Morogoro.
Ofisi ya serikali ya Kijijij cha Mtamba kilichopo Matombo Morogoro. Ni mwendo wa dakika 45 tu kutoka Mtamba mpaka kufika Mlima Chamanyani

photo

Mwanasheria Amani Mwaipaja akitoa mafunzo kwa Wasaidizi wa kisheria
Mwanasheria Amani Mwaipaja (Kulia) akiwa na Mwanasheria Cazimir baada ya kuhitimisha ratiba ya mafunzo

photo

Washiriki wa mafunzo ya Wasaidizi wa Sheria kutoka kata Nne za Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro (Mvuha, Mkuyuni, Mngazi na Mtamba) wakiwa katika picha ya pamoja na Mwanasheria na Mtafiri Amani Mwaipaja wakati wa Mafunzo
 Moja ya Mabango yakionekana kwenye ukumbi wakati wa Mafunzo
Mwanasheria Cazimir (Wa kwanza kushoto) akiwa kwenye picha ya Pamoja na Viongozi wa Vituo vya Wasaidizi wa Sheria Morogoro Vijijini)

photo


 Njiani kuelekea Kata ya Mvuha iliyopo katika Wilaya ya Morogoro (Vijijini)


 Mwanasheria Amani Mwaipaja akiwa kwenye bodaboda kuelekea kitongoji cha Changarawe kilichopo katika kijiji cha Mvuha.
 Mwanasheria Amani Mwaipaja akiwa katika picha ya pamoja na Aliyekua Mwenyekiti wa Kijiji cha Mvuha (Morogoro Vijijini)Bwana Nyandikira muda mfupi baada ya kuwasili Katika kata ya Mvuha

 Jengo la Ofisi ya Kata ya Mvuha likionekana kwa mbali


 Mto Mvuha (Uliopo Morogoro Vijijini) ukiwa umefurika katika kipindi hiki cha msimu wa mvua


Washiriki wakiwa katika majadiliano ya vikundi wakati wa semina

Habari Kamili
Mwanasheria na Mtafiti Amani Mwaipaja  ameanzisha program ya msaada wa kisheria kwa jamii iishiyo pembezoni mwa nchi ya Tanzania (Vijijini) Kwa lengo la Kuhamasisha Vijana-Wasomi kutumia Elimu na Rasilimali walizonazo katika kufanya kazi za kujitolea kusaidia jamii. Program hiyo imepewa jina la Jamii Kwanza.

Program ya Jamii Kwanza inatoa semina, mafunzo na kusambaza elimu kwa njia ya vitabu ili kuhakikisha kuwa jamii kubwa iishiyo vijijini inatambua haki mbalimbali ilizo nazo kwa mujibu wa sheria za Tanzania

photo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kumkaribisha Kaimu Kamishna Jenerali wa TRA, Risherd Badei, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, kwa mazungumzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Kaimu Kamishna Jenerali wa TRA, Risherd Badei, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, Feb 18, 2014 kwa mazungumzo. Picha na OMR

photo ,


 Dr Ellen Otaru Okoedion Private Sector Development Programme 2013 Team leader from Tanzania, takes participants through a new website- www.fanyabiasharatanzania.com- launch in Dar es Salaam to help local entrepreneurs formalize and grow their businesses. 
 Dr Ellen Otaru Okoedion Private Sector Development Programme 2013 Team leader from Tanzania, introducing her teammates who also participated in the launch of a new website-www.fanyabiasharatanzania.com- to help local entrepreneurs formalize and grow their businesses. The ceremony was held in Dar es Salaam at the weekend. 
 Malena Rosman, Head of Development Cooperation Division in the embassy of Sweden (holding a flower boutique and wearing a red jacket) in a group photo with Private Sector Development (PSD) Programme 2013 Team shortly after their graduation and launch of a website to  help local entrepreneurs formalize and grow their businesses. Far left is Julia Norinder and far right is Daniel Stendahl PSD Programme Tutors.
 Daniel Stendahl (right) Private Sector Development (PSD) Programme Tutor says a word of thanks after being awarded by the 2013 PSD team who graduated in Dar es Salaam at the weekend and launched a new website- www.fanyabiasharatanzania.com- to help local entrepreneurs formalize and grow their businesses. Left is Julia Norinder also a PSD programme tutor.
 Julia Norinder (second left) and Daniel Stendahl, Private Sector Development (PSD) Programme Tutors being awarded by the 2013 PSD team who graduated in Dar es Salaam at the weekend and launched a new website- www.fanyabiasharatanzania.com- to help local entrepreneurs formalize and grow their businesses. 

Julia Norinder (second left) and Daniel Stendahl, Private Sector Development  (PSD) Programme Tutors being awarded by the 2013 PSD team who graduated in Dar es Salaam at the weekend and launched a new website- www.fanyabiasharatanzania.com- to help local entrepreneurs formalize and grow their businesses. 

 Private Sector Development (PSD) Programme Country focal point, Emmanuel Nnko shows one of his gifts he received from Tanzania 2013 Private Sector Development team.
 Private Sector Development (PSD) Programme Country focal points, Saada Mufuruki (left) and Emmanuel Nnko (second right) being awarded by the 2013 Private Sector Development team. Kwa picha zaidi Bofya hapa >>>>

photo ,

Mwaka 2009, wazo jipya lilizaliwa. Wazo la kuwa na tuzo zitakazopatikana kwa mchakato wa wazi utakaotokana na mapendekezo ya watu wenyewe ya kuchagua mastaa wa michezo, muziki, filamu au vipindi na watangazaji wanaopendwa zaidi. Wazo hilo liliendelea kuboreshwa na mwaka huu (2014), limeiva na liko tayari kutoka kwenye hatua ya wazo la kichwani, na kuwa tukio lenyewe.

"Nilizisajili na kuanzisha mwaka 2009 ila kutokana na mipango na malengo ya kampuni niliamua kuziweka kwanza hadi sasa," anasema Mwenyekiti wa Bongo5 Media Group, Luca Neghesti.

"Sasa hivi tumeshuhudia ukuaji katika tasnia mbalimbali na tumeona ni wakati muafaka wa kuwatunuku wale wanaopendwa na wananchi, kuwapatia tuzo pamoja na zawadi ya fedha taslimu milioni 1" ameongeza.

Tofauti na tuzo zingine, tuzo za watu hazitafuti ubora bali zinalenga wanaopendwa zaidi na tuzo hizi hazitajikita katika tasnia moja peke yake.

Kwa kuanzia, tuzo hizi zitatolewa katika tasnia ya burudani inayojumuisha filamu na muziki. Pia zitaiangazia sekta ya utangazaji kwa kuwatunuku watangazaji na vipindi vinavyopendwa zaidi na watu nchini huku pia mwanamichezo bora (soka, basketball, ndondi na michezo mingine) naye akipewa nafasi.

Tuzo za watu si tuzo za vijana peke yake, zipo kuwakilisha watu wa rika zote.

Tofauti nyingine kubwa ni kuwa tuzo za watu zitalenga kuwatunuku watu kutokana na umaarufu ama kupendwa kwao na si ubora. "Tuzo hizi hazileti ushindani na tuzo zingine kwasababu hazilengi tasnia moja tu," anafafanua Neghesti.

"Tanzania imesifiwa kwa uhuru wa vyombo vya habari na tuzo hizi zinalenga kujumuika na tuzo zingine kuhakikisha watanzania wanaopendwa na kufanya vizuri wanatambuliwa."

Upigaji kura unaanza wiki hii katika vipengele 11 ambapo wananchi wenyewe watachagua majina ya washiriki watakaoshindana kwenye vipengele hivyo. Awamu ya kwanza ya upigaji kura itafungwa baada ya wiki mbili kutoka siku ya kwanza ya upigaji kura na majina ya watu watano waliotajwa zaidi kutoka kwenye kila kipengele watachaguliwa kama watajwa wa mwisho.

Kuanzia hapo, upigaji kura wa wananchi utajikita tu katika orodha ya majina hayo matano kwenye kila kipengele kinachoshindaniwa. Wiki moja baada ya majina ya washiriki kutangazwa, mchujo wa kwanza utafanyika katika kila kipengele na mtu mmoja ataondolewa.

Wiki moja baadaye, mchujo wa pili utafanyika na kuwabakiza washiriki watatu kwenye ila kipengele.

Washiriki wote 33 (watatu katika kila kipengele) waliosalia baada ya kufanyika mchujo wa mwisho, watakuwa wageni wa heshima kwenye utoaji wa tuzo hizo, utakaofanyika wiki moja baada ya mchujo huo wa mwisho.

Katika hafla hiyo, washindi watatangazwa na kila mshindi atapokea zawadi ya fedha taslimu, shilingi 1,000,000 za Kitanzania pamoja na tuzo ya thamani iliyotengenezwa kwa mkono kutoka kwenye mali ghafi asili za Kitanzania.

Tuzo za watu mwaka 2014 zitajumuisha vipengele 11 ambavyo ni pamoja na:

1. MTANGAZAJI WA REDIO ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW1 na jina' kwenda 15678)
2. KIPINDI CHA REDIO KINACHOPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW2 na jina' kwenda 15678)
3. MTANGAZAJI WA TV ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW3 na jina' kwenda 15678)
4. KIPINDI CHA TV KINACHOPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW4 na jina' kwenda 15678)
5. MWANAMICHEZO ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW5 na jina' kwenda 15678)
6. MWANAMUZIKI WA KIUME ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW6 na jina' kwenda 15678)
7. MWANAMUZIKI WA KIKE ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW7 na jina' kwenda 15678)
8. WIMBO UNAOPENDWA (2013) (tuma SMS yenye 'TZW8 na jina' kwenda 15678)
9. MUIGIZAJI WA FILAMU WA KIUME ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW9 na jina' kwenda 15678)
10. MUIGIZAJI WA FILAMU WA KIKE ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW10 na jina' kwenda 15678)
11. FILAMU INAYOPENDWA (2013) (tuma SMS yenye 'TZW11 na jina' kwenda 15678) JINSI YA YA KUPIGA KURA

Mchakato wa kupendekeza majina ya washiriki katika tuzo hizi utafanyika kwa njia kuu mbili. Ya kwanza ni kwa kutumia tovuti ya tuzo hizi ambayo ni www.tuzozetu.com ambapo utakutana na hatua rahisi ya kupendekeza na kutaja majina katika vipengele vyote 11. Jinsi ya kupiga kura, bofya palipoandikwa Piga Kura na ufuate hatua rahisi kabisa ambayo haikuhitaji kujiandikisha jina wala email yako.

Njia ya pili ni kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu ambapo utaandika neno ‘Tuzo’ kwenda namba 15678. Ukishafanya hivyo utaletewa Menu yenye vipengele vyote 11 vikiwa na code number zake. Kutaja ama kupendekeza jina, tuma code husika na jina kwenye namba hiyo hiyo; kwa mfano Justin Bieber. Gharama ya sms ni ile ile inayotozwa sms ya kawaida.

photo ,

 Mwenyekiti wa Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Mh. George Kahama (liesimama) akitoa muongozo wa namna vikao vitakavyokuwa vinaendelea kufanyika katika kumbi mbali mbali ndani ya Hoteli ya Malaika,iliwa ni muendelezo wa Kongamano Uwekezaji Kanda ya Ziwa,unaoendelea kufanyika kwenye Hoteli ya Malaika,Jijini Mwanza.Wengine pichani toka kushoto ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Titus Kamani,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye ndie Mwenyeji wa Kongamano hilo,Mh. Everist Ndikilo,Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh. Charles Kitwanga pamoja na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mh. Christopha Chiza.
Mwenyekiti wa Kikao kinachojadili maswala ya Ufugaji katika Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Titus Kamani (katikati) akizungumza na Wajumbe wa Kikao hicho (hawapo pichani) wakati akitoa muongozo wa kikao hicho kinachoendelea kufanyika hivi sasa katika Ukumbu wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika,jijini Mwanza.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mh. Said Magalula na Kulia ni Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Bw. Fanuel Lukwaro
Mtoa Mada iliyohusu Fursa za Uwekezaji katika Ufugaji na Michakato ya kuwa na Machinjio bora,Prof. Lazaro Kurwijila kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine (Idara ya Sayansi ya Wanyama) akisisitija jambo wakati akiwasilisha mada yake hiyo,kwenye Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,linaloendelea kufanyika hivi sasa kwenye Ukumbu wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika,jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye ndie Mwenyeji wa Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Mh. Everist Ndikilo akifatilia kwa makini kikao hicho kinachoendelea kufanyika hivi sasa katika Ukumbu wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika,jijini Mwanza.
Wajumbe wakifatilia kikao hicho.
Mwenyekiti wa Kikao kinachojadili maswala ya Kilimo katika Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mh. Christopha Chiza (kulia) akizungumza na Wajumbe wa Kikao hicho (hawapo pichani) wakati akitoa muongozo wa kikao hicho kinachoendelea kufanyika hivi sasa katika Ukumbu wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika,jijini Mwanza.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinganga,Mh. Yohana Balele.
Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),Mh. Aggrey Mwanri (wa pili kulia) akiwa pamoja na Wajumbe wengine kufatilia moja ya vikao vinavyoendelea kwenye Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,linaloendelea kufanyika hivi sasa kwenye Ukumbu wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika,jijini Mwanza.
Wajumbe wakipitia makabrasha mbali mbali ya Kongamano hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii nchini (TTB) Dkt. Aloyce Nzuki (kushoto) akizungumza wakati akiwasilisha mada yake iliyohusu uwepo wa Fursa za Uwekezaji katika Uwindaji na Hoteli wakati wa Kikao kilichokuwa kikijadili maswala ya Miundombinu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Elimu na Afya katika Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,linaloendelea kufanyika hivi sasa kwenye Ukumbu wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika,jijini Mwanza.Picha na Othman Michuzi,Mwanza.

photo ,

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza  na viongozi wa  Jumuiya  za Wafanyabiashara wa kati wa Kariakooo na Mikoani kuhusu mgogoro wa matumizi  ya mashine za TRA, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Feb 12, 2014- usiku.Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha, Adam Malima. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Baadhi ya viongozi wa Jumuiya za wafanyabiashara wa kati wa Kariakoo na Mkoani  wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipozungumza nao kuhusu mgogoro wa matumizi  ya mashine  za TRA, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Februari 12, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na viongozi wa  wa Kampuni ya China ya  AVIC Group China  Civil Aviation inayopkusudia kuwekeza katika kampuni ya  Ndgege ya ATCL, Ofisini kwake jijini Dar es salaam, Februari 13, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

photo ,