Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo TTCL,Bwa.Peter Ngota akionesha kipeperushi chenye taarifa mbalimbali kuhusiana na huduma yao mpya iliyojulikana kwa jina la Bwerere,Kwa waandishi wa habari,huduma hiyo imezinduliwa leo kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Ofisi za kampuni hiyo,zilizopo makao makuu mtaa wa Samora Jijini Dar. 
 Baadhi ya Wandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa huduma mpya ya TTCL iliyojulikana kwa jina la Bwerere ,kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Ofisi za kampuni hiyo,zilizopo makao makuu mtaa wa Samora Jijini Dar. 
Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo TTCL, Bwa.Peter Ngota akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa mkutano wa uzinduzi wa huduma yao mpya iliyojulikana kwa jina la Bwerere,kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Ofisi za kampuni hiyo,zilizopo makao makuu mtaa wa Samora Jijini Dar.

=======  ======= =======

HOTUBA KUHUSU UZINDUZI WA  BWERERE TAREHE 07/08/2014, UKUMBI WA MKUTANO.

Kwa jina: Peter Ngota – Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo TTCL
Ndugu, wanahabari kutoka vyombo mbalimbali,
Ndugu  Waalikwa, Wafanyakazi Wenzangu wa TTCL na Watanzania wote

Habari za asubuhi.

Natumia fursa hii kuwakaribisha  wanahabari, wageni waalikwa na wafanyakazi wenzangu wa TTCL katika ukumbi huu ambapo  leo tuna tukio  muhimu la uzinduzi wa huduma mpya inayo waleta watu karibu zaidi. Ninayo furaha kubwa katika siku hii ya  pekee kuujulisha umma kuwa TTCL inatoa fursa kwa wateja wake  na umma kwa ujumla kutumia mtandao wa TTCL  kupata huduma ya mawasiliano BORA ya simu na intaneti kwa bei nafuu zaidi.  

Ndugu wanahabari ,
Siku ya leo ,TTCL inazindua rasmi promotion inayolenga kuwapa wananchi huduma bora na za bei nafuu. Promotion hii inajulikana kwa jina la  BWERERE   yaani pata huduma nyingi zaidi kwa bei nafuu zaidi.

Promosheni hii inatoa fursa kwa wateja wa majumbani na maofisini ambao wanatumia  huduma ya malipo ya kabla(pre-paid) kufurahia gharama ya viwango vya chini kabisa vya kupiga simu TTCL kwenda kwenda mitandao mingine yote ikiwa ni pamoja na TTCL yenyewe.

Vilevile Promosheni hii inatoa fursa maalumu kwa watumiaji wa vifurushi vya intaneti(DATA)  kwa njia ya Broadband mtandao wa Nyaya na Mkongo waTTCL kitaalamu Fixed lines kuweza kupata intaneti bila kikomo.

Ndugu wanahabari, Wageni waalikwa
Mbali na hayo Promosheni hii ya BWERERE inatoa fursa kwa mteja kupata huduma mbalimbali; Muda wa maongezi wa BURE na Data kwa wakati mmoja na kwa bei nafuu sana.

Huduma hizo ni kama zifuatazo;
·       Tsh 1 kwa sekunde:- Mteja atapata fursa ya kupiga simu  kwenda mitandao mingine kwa shilingi 1 kwa sekunde. Huduma hii haina kujiunga. Kabla ya hapo, kupiga simu TTCL kwenda mitandao mingine ilikuwa ikigharimu Tsh 230 kwa dakika 1. Kwa sasa mteja wa TTCL ataweza  kupiga simu katika mitandao mingine na kuweza kuongea na ndugu, jamaa na marafiki kwa Tsh 1 moja kwa sekunde yaani kwa gharama ya shilingi sitini kwa dakika 1; Sawa na punguzo la Asilimia zaidi ya 70%

·       Bwerere Premium:- inahusisha wateja wanaotumia huduma ya intaneti kuanzia kiwango cha 2Mbps  mpaka 32 GB watapata fursa kupiga simu TTCL  kwenda TTCL  bure ndani ya mwezi, pia mteja atapata muda wa maongezi  kuanzia dakika 300 mpaka dakika 600 kupiga simu kwenda mitandao mingine ndani ya mwezi.

·       Bwerere Unlimited:- huduma hii inahusisha watumiaji wa intaneti kuanzia kiwango cha 512Kbps mpaka 2Mbps watapata huduma ya muda wa kupiga simu bure TTCL kwenda TTCL kwa muda wa mwezi mzima.

·       Bwerere:- kwa watumiaji wa intaneti njia ya Broadband kuanzia 3 GB mpaka 24 GB watapata fursa ya kupiga simu bure TTCL kwenda TTCL.

Tunaendelea Kupanua Wigo wa uchaguzi wa huduma za vifurushi kwa watumiaji na kuwapa fursa ya waTanzania kutumia huduma za TEHAMA kwa bei nafuu kwa maendeleo ya M-Tanzainia na Taifa.

Ndugu wanahabari
TTCL inapenda kuutarifu umma faida za simu za mezani, Simu za mezani katika mawasiliano na maendeleo kwa ujumla kama ifuatavyo;
1.     Simu za mezani zinausalama mkubwa sio rahisi kwa mtu kuingilia mawasiliano ambayo yanatolewa kwa njia ya waya yaani kitaalamu cable.

2.     Vilevile simu za mezani  ni nzuri sana kwa matumizi ya kiofisi na majumbani, ni rahisi kutambua sehemu ya ofisi au nyumba unayoishi, pia Ni simu ambazo zinakuthibitishia uwepo wa mtu unayewasiliana naye katika eneo husika.

3.     Mwisho, simu za mezani  mawasiliano yake yana ubora mkubwa na uhakika kiusikivu na kasi zaidi kwa intaneti.

Napenda kuitimisha kwa kuwakaribisha wateja wote, na  ninyi wanahabari kufurahia huduma hii ya BWERERE ambayo inakupa huduma nyingi kwa wakati mmoja.

TTCL ni kampuni pekee hapa nchini ambayo inatoa huduma za DATA, simu zenye ubora zaidi. Ni mtandao pekee ambao umeenea katika mikoa na wilaya zote nchini.

Sasa ni wakati mzuri wa kutumia na huduma hii ya BWERERE na Ufaidike zaidi na TTCL kwa UBORA wa huduma na gharama nafuu zaidi nchi nzima.

TTCL HULETA WATU KARIBU.
Na sasa niwakaribishe wataalamu wetu kwa maelezo zaidi

Asanteni kwa kunisikiliza

Peter Ngota
AFISA MKUU WA MASOKO NA MAUZO.

photo ,

0 Responses so far.