Waendeshaji wa Show ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Joti na Lulu wakiwa kwa steji, tayari kwa kuendelea na show hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Mkaumbusho ya Taifa Jijini Dar Es Salaam.
 Mshiriki Ally Kiwendo ambae alikuwa ni mmoja kati ya washindi watatu kutoka kanda ya Kusini mkoani Mtwara akitoa maneno ya shukrani kwa Kampuni ya Proin Promoitons ambao ndio waandaaji na waendeshaji wa Shindano la TMT mara baada ya kutangazwa kuaga shindano hilo kutokana na Kura kuwa chache, huku pia akiwashukuru watazamaji na wote waliompigia kura
 Joyce Kalinga Mshiriki wa Shindano la TMT ambae apia alikua mshindi kutoka Kanda ya Kati Mkoani Dodoma akitoa maneno yake ya shukrani na pia kuwashukuru wadau, Kampuni ya Proin Promotions na watazamaji na waliompigia kura japokuwa bahati haikuwa yake kutokana na kutolewa kwenye kinyanganyiro hiko kutokana na uchache wa kura kutoka kwa watazamaji
 Lulu na Joti wakitoa maelekezo kwa washiriki wawili wa Shindano la TMT ambao waliweza kutolewa katika kinyanganyiro hiko kutokana na kupata kura chache kutoka kwa watazamaji wa Kipindi cha TMT kinachorushwa Kila Jumamosi saa Nne usiku.
Baadhi ya washiriki wakiwa na nyuso za simanzi kutokana na Washiriki wenzao wawili kuaga mashindano hayo.Picha zote na Josephat Lukaza.
Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited - Dar Es Salaam.
Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Linaelekea Ukingoni ambapo mwisho wa Mwezi huu wa nane Mshindi mmoja wa shindano hilo la TMT ataondoka na kitita cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania katika fainali kubwa.
 Shindano la TMT ni shindano ambalo limekuwa likiteka hisia za washiriki pamoja na wadau na watazamaji wa kipindi hiko cha TMT ambacho kimejizolea umaarufu nchini na nje ya Nchini kutokana na Umahiri wake ambapo awali shindano hilo lilianza kanda ya ziwa Mkoani Mwanza kwaajili ya kusaka vipaji vya kweli vya kuigiza ambapo baadae safari ilielekea katika kanda nyingine za Tanzania ambapo washindi watatu kutoka kila kanda waliweza Kupatikana na hatimaye kufanya jumla ya washiriki ishirini kutokana kanda sita za Tanzania Kuwasili Jijini Dar Es Salaam, Mwishoni mwa Mwezi wa Sita ambapo waliweka kambi na kuanza kupewa mafunzo na Mwalimu Kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam aitwaye Dk Mona Mwakalinga akisaidia na Mwl Issa.
Washiriki Hao 20 waliweza pia kupata fursa ya kufanya filamu fupi ambazo ziliweza kupima uwezo wao wa kuigiza mara baada ya kutoka darasani na hatimaye kupelekea watazamaji kuweza kuwapigia kura huku wakisaidiana na majaji wa Shindano hilo. Majaji wa shindano hilo ni Roy Sarungi, Vyonne Cherry na SIngle Mtambalike.
Mpaka sasa Jumla ya Washiriki 7 wameshatoka kwenye kinyanganyiro na kupelekea kubaki na washiriki wengine 13 ambapo washiriki watatu wanatakiwa kutoka na kubaki washiriki 10 huku kumi hao wakiwa wameingia fainali sasa ya kuzisaka zile Milioni hamsini ambazo Mshindi mmoja atajinyakulia siku ya Fainali inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Mwezi wa 8.
Ili kuweza kumbakiza mshiriki wako unachotakiwa kufanya ni Kumpigia Kura kwa wingi kupitia Simu yako ya mkononi kwa kuandika Neno "TMT" acha nafasi namba ya Mshiriki halafu tuma kwenda 15678. Mfano "TMT" 00 halafu tuma kwenda 15678 au Pia unaweza kumpigia kura mshiriki umpendae kupitia ukurasa wetu wa facebook kwa kutembelea anuani ifuatayo https://www.facebook.com/tztmt.
Washiriki Kumi watakaoingia Kwenye Fainali ya Kusaka Milioni 50 watakuwa chini ya Kampuni mahiri ya Utengenezaji na Usamabazaji wa filamu za Kitanzania ya Proin Promotions ambao ndio waandaaji na waendeshaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents, Shindano Bora na kubwa Tanzania na la Kwanza kufanyika Afrika Mashariki na Kati

photo ,

0 Responses so far.