Kaimu
Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Jasper Mero
(Mbele) akiingia katika ukumbi wa Kings way kufungua mafunzo ya awali
(Induction course) kwa waajiriwa wapya wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi
yanayofanyika katika Hoteli ya Kings Way Mkoani Morogoro.
Mkurugenzi
Msadizi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi,
Bibi Eliaika Manyanga (Kulia) akizungumza na waajiriwa wapya wa Ofisi
hiyo katika mafunzo ya awali (Induction course) yanayofanyika katika
Hoteli ya Kings Way Mkoani Morogoro.
Baadhi
ya waajiriwa wapya wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wakiwa katika mafunzo
ya awali (Induction course) yanayofanyika katika Hoteli ya Kingsway
Mkoani Morogoro.
Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali Watu wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Bw. Gerald
Mwanilwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa
ufunguzi wa mafunzo ya awali ya waajiriwa wapya wa Ofisi hiyo jana Mjini
Morogoro.
Kaimu
Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Jasper Mero
(Kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa mafunzo
ya awali kwa waajiriwa wapya wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi yanayofanyika
katika Hoteli ya Kingsway Mkoani Morogoro.
Baadhi
ya waajiriwa wapya wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wakimsikiliza kwa
umakini Kaimu Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw.
Jasper Mero (hayupo pichani).
Kaimu
Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Jasper Mero
(Kushoto) akisisitiza jambo wakati akijibu maswali mbalimbali ya
waajiriwa wapya wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.
Kaimu
Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Jasper Mero
(Katikati waliokaa) na baadhi ya viongozi waandamizi wa Ofisi ya Taifa
ya Ukaguzi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waajiriwa wapya wa
Ofisi hiyo.
PICHA ZOTE NA SAIDI MKABAKULI.
Na Saidi Mkabakuli
Watumishi wa umma nchini wameaswa kuwa waadilifu na kuzingatia ubora wa kazi wakati wanatoa huduma kwa wananchi.
Wito
huo umetolewa na Kaimu Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali,
Bw. Jasper Mero wakati akifungua mafunzo ya awali ya wiki moja kwa
waajiriwa wapya 130 wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi yanayofanyika katika
Hoteli ya Kingsway mkoani Morogoro.
Bw.
Mero amesema kuwa udilifu na ubora kwa watumishi wa umma ni kinga dhidi
ya matumizi mabaya ya ofisi za umma na ni moja kati ya njia
zinazowawezesha watumishi wa umma kuwa wachapakazi hodari.
“Ofisi
ya Taifa ya Ukaguzi inaamini katika “Ubora”kwa kila inachokifanya
ukianzia ubora wa taarifa za ukaguzi zinazotolewa, huduma bora kwa wadau
wake, ubora wa watumumishi kwa maana ya taaluma, maadili, weledi,”
alisema Bw. Mero.
Ameongeza kuwa Falsafa hii ya ubora ndiyo iliyoifanya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kupata umaarufu mkubwa kikanda na Kimataifa.
“Kiwango
cha juu cha Ubora wa kazi zetu na utendaji wa kazi unaozingatia weledi
vitaweza tu kufikiwa kwa kuajiri watumishi wenye sifa stahiki, maadili,
na bidii ya kuchapa kazi na wanaoweza kwenda sambamba na kasi kubwa ya
mageuzi katika Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi,” aliongeza Bw. Mero.
Akizungumza
wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa
Ofisi hiyo, Bw. Gerald Mwanilwa alisema kuwa mafunzo elekezi ni matakwa
ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za mwaka 2003, hususani Kanuni
Na.103 (1-6) pamoja na Kanuni za kudumu za Utumishi Serikalini za 2009
Kifungu G.3 (a na b).
“Mafunzo
haya ni kwa mujibu wa matakwa ya kisheria na yanalenga kutoa uelewa
mahususi kwa waajiriwa wapya kulingana na kada zao,’ alisema.
Kwa
mujibu wa Bw. Mwanilwa, kupitia mafunzo hayo, washiriki wataweza kuelewa
namna ya kutekeleza majukumu yao kama Watumishi wa Umma pamoja na
kupata fursa ya kujifunza Miongozo na Nyaraka mbalimbali watakazozitumia
kama watumishi wa umma na wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa
Hesabu za Serikali.
Pia,
kupitia mafunzo hayo watapata fursa ya kujifunza na kuelewa utamaduni wa
Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi unaosisitiza kufanya kazi kwa uweledi,
uadilifu na kwa kuzingatia ubora na viwango vya kitaifa na kimataifa
ambapo ofisi yetu ni Mwanachama (Intosai Afrosai na Afrosai-E).
“Mafunzo
haya ni ya wiki moja yatatoa fursa kwenu kujua maana ya kuwa mtumishi
na kazi za mkaguzi na miiko au maadili yake. Pia mtaelezwa kwa kifupi na
kupewa utangulizi kuhusu Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, sheria mbali mbali,
Kanuni na taratibu ili kuwawezesha kuelewa na kufanyakazi kama
watumishi wa umma,” aliongeza Bw. Mwanilwa.
0 Responses so far.
Post a Comment