DSC_0083
Mshehereshaji ambaye ni Mwanakamati ya maandilizi ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014, Usia Nkhoma Ledama akiwatambulisha baadhi ya waandishi wa habari wakongwe (hawapo pichani) kwa mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mark Bomani.(Picha zote na Zainul Mzige).
Na Mwandishi wetu
Jaji Mstaafu Mark Bomani amesema lengo la mchakato wa Katiba ni kuhakikisha kwamba Tanzania inapata Katiba ambayo ni bora zaidi kuliko zote itakayoshughulikia changamoto na kuweka mazingira ambayo yatamrahisishia maendeleo mwananchi kwa haraka.
Akitoa risala katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani leo katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC jijini Arusha, Jaji Mstaafu Mark Bomani, amesema jukumu la mwanahabari ni kuwaelimisha baadhi ya wabunge wa Bunge Maalum la Katiba ambao hawana uelewa mkubwa na mchakato wa Katiba hawajui maana halisi ya Katiba mambo ambayo yanasababisha kujadili Katiba hiyo kwa maneno mabaya, kutishiana, matusi na kejeli.
DSC_0171
Baadhi ya waandishi wa habari wakongwe (Ma-veterans) wakimsalimia mgeni rasmi.
“Zoezi la mchakato wa Katiba ni kubwa na wabunge wengi wa Bunge Maalum la Katiba hawaelewi wajibu wao katika kuijadili Katiba hiyo matokeo yake ndio hayo wanayoshuhudia Watanzania”.
Mara nyingi Watanzania wameshuhudia mijadala ya kejeli, malumbano, matusi, kudharauliana pale hoja zinapojengwa na upande ambao haukubaliki na upande mwingine jambo ambalo limewavunja moyo Watanzania na kutokuwa na imani ya kupata Katiba inayolenga kumlinda mwananchi.
Jukumu la wanahabari ni kutoa elimu ya kutosha kuhusu yaliyomo katika Katiba Mpya na kuandika habari za maendeleo ili majadiliano yatokanayo yawe endelevu yamtendee haki mwananchi wa kawaida kwa lengo la kuboresha maisha yao.
DSC_0077
Meza Kuu, kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Elimu, Sayansi na Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa (UNESCO) Bw. Abdul Wahab Coulibaly, Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) Bw. Ernest Sungura, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Bw. John Mongela, Mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mark Bomani, Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Bw. Mohamed Tibanyendera, Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Kenneth Simbaya na Meneja Utafiti na Ushapishaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. John Mirenyi.
“Inasikitisha kuona kuwa hali ya Mtanzania inazidi kudidimia au kubaki pale pale katika sehemu nyingi hasa vijijini katika kipindi cha miaka 40 iliyopita kwa kukosa fursa muhimu za maendeleo na viongozi hawalioni hilo”, amesema Jaji Mstaafu Mark Bomani.
Wakati huo huo mgeni huyo rasmi amekemea tabia ya kuandika habari za kuwasifu viongozi na kupokea Rushwa hali iliyojitokeza katika miaka ya hivi karibuni na kusema kwamba ni fedhea kwa tasnia ya habari kutofuata maadili ya uandishi.
Amesema kwamba nchi itaendeshwa kwa kusimamia haki na ukweli na kuwataka wanahabari wasichoke kuisimamia haki na uhuru wa nchi yao bila woga kwani bila kufanya hivyo nchi itaongozwa kiimla.
DSC_0348
Mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mark Bomani, akitoa risala wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014 yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC jijini Arusha mwishoni mwa juma.
“Kuna tabia ya vyombo vya habari ya vyombo vya habari kununuliwa ili visiandike au kufichua maovu ni fedhea kwani vyombo vya habari ni kioo cha jamii”.
Akizungumzia kuhusu sheria za habari za mwaka 2007 na 2008, Jaji Mstaafu amesema ni aibu kuona mswaada wa sheria ya habari umekwama kwa zaidi ya miaka 10 kwa sababu ambazo hadi leo hazijaeleweka.
Amewataka waandishi wa habari wasikate tamaa na badala yake waendelea na kupambana kuhakikisha kwamba harakati za kupata Sheria ya Haki ya Kujua inafanikiwa ili kupunguza matukio ya manyanyaso, kupigwa, kuteswa, kufungwa kwa vyombo vya habari na kuuwawa.
“Haki haiyombwi simamieni Haki zenu na songeni mbele”, ameongeza Jaji Bomani.
DSC_0429
Sehemu ya wadau wa tasnia ya Habari wakisikiliza risala ya mgeni rasmi.
DSC_0329
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Bw. John Mongela akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa wa Arusha kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika jijini Arusha kenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC.
DSC_0112
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Bw. Mohamed Tibanyendera, akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014 yaliyofanyika kwenye ukumbi wamikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha.
DSC_0163
Wageni waalikwa na wadau wa tasnia ya habari wakiwa kwenye ukimya kumkumbuka Mwandishi aliyeuwawa mkoani Iringa Daudi Mwangosi.
DSC_0188
Mkurugenzi wa Shirika la Elimu, Sayansi na Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa (UNESCO) Bw. Abdul Wahab Coulibaly, akitoa Ujumbe wa Pamoja wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Irina Bokovas kuhusiana na Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014.
DSC_0217
Meneja Machapisho, Utafiti na Uhifadhi Hati wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. John Mirenyi, akitoa maelezo ya machapisho mbalimbali yaliyoandaliwa na baraza hilo yakiwemo yenye madhila mbalimbali yaliwahi kuwakumba baadhi ya waandishi wa habari ndani na nje ya nchi.
DSC_0241
Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) Bw. Ernest Sungura, akizungumzia mchango wa mfuko huo unaowawezesha waandishi wa habari kutafuta habari za uchunguzi na zinazoigusa jamii.
DSC_0247
Wasanii wa Bendi ya Mrisho Mpoto (Mjomba Band) wakitoa burudani kwa wageni waalikwa wakati wa maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014 yaliyofanyika jijini Arusha mwishoni mwa juma.
DSC_0156
Sehemu ya wadau wa tasnia ya habari wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini hapo.
DSC_0259
Katibu wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT), Henry Muhanika, akisoma hotuba kwa niaba ya Dr. Reginald Mengi kwenye maadhisho hayo.
DSC_0269
Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Kenneth Simbaya, akizungumzia wakati wa maadhimisho hayo.
DSC_0286
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda, akizungumzia changamoto mbalimbali zinazowakumba waandishi wa habari wakati maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014 yaliyofanyika jijini Arusha.
DSC_0288
Mkurugenzi wa TAMWA, Bi. Valerie Msoka, akizungumzia changamoto za usawa wa Kijinsia katika uongozi kwenye Vyombo vya Habari nchini.
DSC_0304
Meneja Uhusiano wa TANAPA, Pascal Shelutete, akizungumzia ushiriki wao kwenye Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014 ambapo aliwataka waandishi wahabari kutumia kalamu zao vizuri katika kukuza Utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi.
DSC_0312
Meneja Uhusiano wa Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, Bw. Adam Akyoo, akifafanua jambo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014 ambapo amewataka waandishi wa habari kutumia nafasi yao katika kupambana na suala la Ujangili linaloendelea nchini.
DSC_0382
Mrisho Mpoto akiwafungua vitambaa wasaani wa Mjomba Bendi kama ishara ya kuwapa Uhuru waandishi wa Habari kuzungumza kilio chao mbele ya mgeni rasmi kama ujumbe wa Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014.
DSC_0398
Mrisho Mpoto na Bendi yake akighani mashairi na kuelezea madhila wayapatayo waandishi wa habari wawapo kazini ikiwemo usalama wao katika kazi zao za kila siku.
DSC_0405
Makamu wa Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC), Jane Mihanji akimkaribisha mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mark Bomani kuzindua Video mpya ya wimbo "Uhuru Wangu" wa Mrisho Mpoto uliokuwa kwenye Albamu yake mpya inayoitwa WAITE.
DSC_0414
Mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mark Bomani, akibonyeza kitufe kuzindua rasmi wimbo huo wakati maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014.
DSC_0422
Wageni waalikwa wakitiza wimbo huo.
DSC_0466
DSC_0497
DSC_0052
DSC_0547
Mkurugenzi wa Mbeya Highlands FM, Bi. Jacqueline Mwakyambiki, akishiriki kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo Vya Habari Duniani 2014 yaliyofanyika jijini Arusha.
DSC_0445
Mgeni rasmi Jaji Mark Bomani akizindua Album mpya ya Mrisho Mpoto inayoitwa "WAITE".
DSC_0476
Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani Jaji Mstaafu Mark Bomani akizindua na kuonyesha moja ya Ripoti ya Unyanyasaji dhidi ya Uhuru wa Habari iliyoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT). Kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika - Taiw la Tanzania (Misa - Tan), Bw. Mohamed Tibanyendera.
DSC_0493
DSC_0518
MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani, Ahmed Kipozi akiteta jambo na mmoja wa Waandishi wa Habari wakongwe Bw. Salim Salim kutoka visiwani Zanzibar.
DSC_0562
Waandishi wa Habari wakongwe (Ma-Veterans) kutoka kushoto Mama Eda Sanga, Fatuma Aloo na Leila Sheikh wakifurahi jambo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika jijini Arusha .
DSC_0359
Mshauri na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Mama Rose Haji Mwalimu, akisalimiana na Meneja Uhusiano wa Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, Bw. Adam Akyoo wakati maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014 yaliyofanyika jijini Arusha.
DSC_0579
Wadau wa tasnia ya habari wakinunua Album ya msaanii Mrisho Mpoto.
DSC_0572
Baadhi ya wasanii wa Mjomba Band wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mwandishi wa habari mkongwe Leila Sheikh.

photo ,

0 Responses so far.