Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akiwasilisha Bungeni  Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa mwaka wa fedha 2014/2015 mjini Dodoma tarehe 27 Mei 2014
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Rajabu Gamaha (wa kwanza kulia) pamoja na Mke wa Waziri, Mama Dorcas Membe na Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia, Balozi Mohammed Maundi wakifuatilia kwa makini Hotuba ilikuwa ikitolewa na Mhe. Membe (hayupo pichani) Bungeni.
Katibu Mtendajii wa Jumuiya ya Maedneleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika, Dkt. Stergomena Tax (katikati) akiwa na wageni wengine wakifutilia Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa mwaka 2014/2015
Baadhi ya Wawakilishi kutoka Balozi za nchi mbalimbali zilizopo hapa nchini wakifuatilia Hotuba ya Mhe. Membe (hayupo pichani)
Baadhi ya Wanafunzi kutoka Vyuo Vikuu vya Mzumbe, SAUT, UDSM, UDOM na CFR wanaochukua Kozi za Uhusiano wa Kimataifa wakifuatilia hotuba ya Mhe. Membe.
Baadhi ya Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakifuatilia hotuba ya Mhe. Membe

Watendaji  kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakifuatilia hotuba.
Watendaji wengine kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakifuatilia Hotuba ya Mhe. Membe.
Wajumbe wakimsikiliza Mhe. Membe
Mwakilishi kutoka Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Betty Machangu (Mb.) akiwasilisha Hotuba kwa niaba ya Kamati hiyo
Mhe. Membe (kushoto) akiwa na Naibu wake Mhe. Dkt. Mahadhii Juma Maalim (Mb.) wakifuatilia hotuba wakati Mhe. Machangu (hayupo pichani) akiwasilisha
Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje kutoka Kambi ya Upinzani, Mhe. Ezekiel Wenje nae akiwasilisha hotuba ya kambi yake.
Mhe. Membe akiongozana na Mhe. Wenje kutoka Bungeni mara baada ya kipindi cha mchana kumalizika.
Mhe. Membe, Mama Dorcas Membe (wa nne kutoka kushoto) katika picha ya pamoja na Dkt. Tax  wakiwa nje ya Viwanja vya Bunge mara baada ya kipindi cha mchana kumalizika

photo ,

0 Responses so far.