Afisa Mwandamizi Uraghibishi wa Ushindani,Alex
Mbaga akizungumza kwenye semina hiyo leo kwa wataalamu wa manunuzi na
ugavi kutoka taasisi mbalimbali juu ya manunuzi yanayozingatia thamani
(Value for Money) iliyofanyika kwenye hotel ya Tanga Beach Resort
mjini hapa.
Mkuu wa Idara ya Cartels (Makubaliano
yanayodhirisha ushindani) kutoka Tume ya Ushindani Dar es
Salaam,Shedrack Nkelebe akisisitiza jambo kwenye semina hiyo
iliyohusisha wataalamu wa manunuzi na ugavi kutoka taasisi mbalimbali
juu ya manunuzi yanayozingatia thamani (Value for Money) iliyofanyika
kwenye hotel ya Tanga Beach Resort mjini hapa.
wataalamu wa manunuzi na ugavi
kutoka taasisi mbalimbali nchini wakifuatilia semina ya juu ya
manunuzi yanayozingatia thamani (Value for Money) iliyofanyika kwenye
hotel ya Tanga Beach Resort mjini hapa
Wataalamu wa manunuzi na ugavi
kutoka taasisi mbalimbali nchini wakifuatilia semina ya juu ya
manunuzi yanayozingatia thamani (Value for Money) iliyofanyika kwenye
hotel ya Tanga Beach Resort mjini hapa
Washiriki wa semina hiyo wakiwa kwenye
picha ya pamoja leo iliyofanyika kwenye hotel ya Tanga Beach Resort
mjini hapa
Washiriki wa semina hiyo wakiwa kwenye
picha ya pamoja leo iliyofanyika kwenye hotel ya Tanga Beach Resort
mjini hapa
Bi Martha Mapalala kutoka mmoja wa waratibu wa semina hiyo inayofanyika mkoani Tanga.
...................................................................................
NA MWANDISHI WETU,TANGA
MAAFISA Ugavi nchini wametakiwa kuzingatia ubora wa vitu
vinavyonunuliwa kwenye maeneo yao jambo ambalo litapelekea kuondoka
bidhaa feki kwenye soko.
Wito huo ulitolewa leo na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Noel
Mrope wakati wa semina ya wataalamu wa manunuzi na ugavi kutoka
taasisi mbalimbali juu ya manunuzi yanayozingatia thamani (Value for
Money) iliyofanyika kwenye hotel ya Tanga Beach Resort mjini hapa.
Semina hiyo ilikuwa na lengo la kuwajengea uwezo maafisa hao juu ya
umuhimu wa kufanya manunuzi yanayozingatia thamani halisi ya fedha
iliyoendeshwa na bodi ya taaluma ya manunuzi na ugavi nchini (PSPTB).
“Pamoja na kuzingatia sheria za Manunuzi lakini kwa kinachonunuliwa
kuanzia fedha zilizotumika kwenye manunuzi kwa sababu hali hii
itawezesha kuondoa uwepo wa bidhaa feki zinazosambazwa kwenye masoko
“Alisema Mdhahiri huyo.
Aidha alisema kuwa mambo ya muhimu yaliyotiliwa mkazo kwenye semina
hiyo ni namna ya wataalamu hao kuangalia thamani ya kitu na jinsi gani
kinaweza kutumika katika kupandisha thamani yake na ubora ili mwisho
wa siku watu wengi waweze kukitumia kitu hicho. “Katika jambo hili lazima wataalamu wa manunuzi kuhakikisha kwa
pamoja wanafuata taratibu za manunuzi kwa kuzingatia sheria lengo
likiwa kuona uthamani na ubora wa kitu ikiwemo thamani ya fedha halisi
iliyotumika “Alisema.
Alisema kuwa kuwa kimsingi maafisa hayo wanatakiwa wanapokwenda
kununua vitu wasikimbilie bei ya chini bali waangalie ubora na thamani
ya kitu halisia ili kuweza kuzipa changamoto bidhaa zisizokuwa na
kiwango kukosa soka na hatimaye kuondoka kwenye soko la ushindani.
Hata hiyo alisema kuwa wananchi wanapobaini kuna vitu vimefanyika
kwenye Halmashauri yao chini ya kiwango wanapaswa kulalamika kupitia
maeneo husika ili kuweza kukabiliana na hali hiyo.