Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Damian Lubuva akizungumza wakati wa mkutano na Viongozi wa Vyama vya Siasa uliofanyika  kwenye Ukumbi wa JB Belmonte,Jijini Dar es salaam.Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Julius Malaba na kulia ni Kamishina wa Tume yaTaifa ya Uchaguzi,Prof. Amon Challigha
Sehemu ya Viongozi wa Vyama vya Siasa waliohudhulia Mkutano huo wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Damian Lubuva (hayupo pichani) leo kwenye Ukumbi wa JB Belmonte,Jijini Dar es salaam.
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini,Jaji Francis Mutungi akichangia mada katika mkutano huo wa Viongozi wa Vyama vya Siasa uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa JB Belmonte,Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha UDP,Mh. John Momose Cheyo akiwa na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi CCM,Ndg. Nape Nnauye wakati wa mapumziko mafupi ya mkutano huo.
Mwenyekiti wa CHADEMA,Mh. Freeman Mbowe akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Chama cha ACT,Ndg. Samson Mwigamba.
Eeehh....bwanaaaaa upoooo........?? Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi,Mh. James Mbatia akifurahi jambo na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi CCM,Ndg. Nape Nnauye.Katikati ni Katibu Mkuu wa CHADEMA,Dkt. Wilbroad Slaa.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

photo ,

0 Responses so far.