Mwandishi Maarufu wa vitabu duniani Chinua Achebe amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82. Msemaji wa jimbo la Anambra nchini Nigeria Mike Uda ameiambia BBC kuwa wanaomboleza kifo cha wanayemwita mtoto wa taifa la Nigeria na Afrika kwa ujumla.
 
Chinua Achebe alizaliwa mwaka 1930, miaka 30 kabla ya Nigeria kupata uhuru.
Taarifa iliyotolewa kwa niaba ya familia yake, imemwelezea Chinua Achebe kuwa mmoja wa waandishi wakubwa wa vitabu vya fasihi katika kipindi chake, ambaye busara yake ilikuwa kichocheo cha kumwiga kwa wale wote waliomfahamu.

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan amesema Profesa Achebe ataishi daima katika mioyo ya akili za watu wa kizazi kiliochopo na vijavyo. Alipata umaarufu mkubwa kutokana na utunzi wa kitabu chake cha kwanza cha fasihi kitwaacho 'Things Fall Apart', ambacho alikitunga mwaka 1958 kikizungumzia athari za ukoloni barani Afrika.

Kitabu hiki kiliuza zaidi ya nakala milioni 10. Things Fall Apart kimetafsiriwa katika zaidi ya lugha 50 na kuelekeza mtazamo wake katika jamii ya Wa-Igbo na mgongano wa kimaadili kati ya nchi za mgaharibi na kijadi.

Alipata ngazi ya uprofesa kutoka chuo kikuu cha Boston nchini Marekani mwaka 1970 ambapo katika siku za hivi karibuni alikuwa akikosoa baadhi ya mienendo mibaya ya serikali ya Nigeria.
Amekuwa akiishi nchini Marekani tangu mwaka 1990 kufuatia kujeruhiwa katika ajali ya gari.
Ameandika kazi za kitaaluma zaidi ya 20, baadhi zikikosoa vikali wanasiasa na uongozi mbaya nchini Nigeria.

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan amesema Profesa Achebe ataishi daima katika mioyo na akili za watu wa kizazi kiliochopo na vijavyo.
 CHANZO BBC
 

photo

Kiongozi wa jopo la wanasheria watano (5) wanaomtetea Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Lwakatare, Wakili Tundu Lissu, akiwawakilisha wenzake, ameongea na vyombo vya Habari akiwa Makao Makuu ya CHADEMA na kuzungumzia masuala kadhaa kutokana na sakata hili.

Lengo kuu la mkutano huo na wanahabari lilikuwa ni kuutarifu umma wa Watanzania kupitia kwa wanahabari juu ya hatua ambayo mawakili hao wameamua kuchukua kwa kupeleka ombi Mahakama Kuu ya Tanzania, chini ya hati ya dharura ili Mahakama hiyo ya juu iitishe mafaili yote mawili yaliyofunguliwa kuhusu kesi ya Lwakatare, yaani faili la kesi iliyofutwa na faili lililofunguliwa baada ya kesi ya awali kufutwa, wakiiomba mahakama iangalie na kujiridhisha…


Kuhusu video
Wanahabari walitaka kujua maoni yake kuhusu video na namna kesi hiyo ilivyo, hasa kutokana na alivyoielezea ‘charge’ ilivyo ‘defective’, ambapo Wakili Lissu kwa maoni yake, alisema kuwa kuna masuala mengi yanatakiwa kuwekwa wazi kuhusu video yake, akihoji maswali kadhaa:


- Nani aliyemrekodi Lwakatare? Je, Lwakatare alijua kuwa anarekodiwa? Je, aliruhusu? Kama hakuruhusu, ilifanyika kihalali? Je, haivunji katiba ya nchi inayozungumzia privacy ya mtu? Je, baada ya kurekodiwa mkanda huo ulipelekwa wapi? Nani alikuwa nao? Je, umefanyiwa uhariri (editing) na nani? Je, aliyemrekodi alitumwa na nani?

Ushahidi mwingine
Ameongeza kuwa, video inaonekana imechukuliwa tarehe 28 Desemba, siku iliyofuata, Desemba 29, kwenye kipindi cha TV, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba akaanza kusema kuwa anayo video ya viongozi wakuu wa CHADEMA wakipanga mipango ya mauaji ya dhidi ya Watanzania.


Amezungumzia mawasiliano ya mtu anayeitwa Michuzi, kuwasiliana na watumishi wenzake wa OBR, akiwapongeza na kutoa kudos kwa TISS kwa kazi nzuri, akiwataka wenzake wapige sana kelele kwani hiyo ni kete muhimu kwa CCM. Amesema kwa mujibu wa Sheria ya Usalama wa Taifa, hawaruhusiwi kufanya surveillance dhidi ya wapinzani wa kisiasa wa CCM, kwa sababu upinzani wa kisiasa ni suala lililoruhusiwa kisheria nchi hii.

Aidha, Lissue ameongeza kusema wamepata mawasiliano ya simu yakionesha kuwa siku hiyo hiyo ambayo video imerekodiwa, majira ya saa 5.59, mtu aitwaye Ludovick alimpigia simu mtu aitwaye Mwigulu Nchemba.

Kwa mujibu wa Wakili Lissu, yamepatikana pia mawasiliano ya mtu aitwaye Dennis Msacky akimpigia simu Lwakatare, ambapo wamemuuliza Lwakatare iwapo ni kweli aliwasiliana na mtu mwenye jina hilo (ambaye kwenye charge sheet ya pili, polisi wameonesha ndiye aliyekuwa akipangiwa kutekwa/kufanyiwa vitendo vya ugaidi), naye amekubali kuwa ni kweli alimpigia simu siku moja kabla ya tukio la kurekodiwa, akimuuliza kama amerudi Dar es Salaam, naye akamwambia alikuwa njiani kutoka Bukoba.

Amemaliza kwa kusema kuwa kesi hii ni kama kesi nyingine za kupikwa, ambazo polisi wamekuwa wakifungua dhidi ya CHADEMA na viongozi wa chama hicho, kwa nia ya kuiokoa CCM, kwasababu chama hicho kimekaliwa vibaya na hakiwezi tena kufanya siasa za ushindani dhidi ya wapinzani wao wakuu, CHADEMA.


===========
Habari hii unaweza kuisoma kwa kirefu -> Sakata la Lwakatare: Wanasheria CHADEMA ‘wafunguka’! | Fikra Pevu

photo

Baadhi ya picha za mastaa wa Bongo katika mikao tofauti ambayo kimsingi inanyemelea kwenda kinyume na maadili ya kitanzania. Bado wasanii wetu wanakabiliwa na changamoto kubwa ya namna ya kudhibiti masuala yao binafsi. Wasanii wengi bado wanatumia mbinu za kizamani za kuuvuta umaarufu kwa kutumia skendo ambazo baadae huwadhalilisha pasipo kuwa na sababu za kufanya hivyo.

 Wasanii wetu wengi hawana uelewa wa kutosha na teknolojia ya sasa. Wanapiga picha, wanajirekodi hata mambo ya faragha na mwisho wake huwa mbaya hasa pale picha na maudhui ya picha hizo zinapovuja na kuifikia jamii ambayo huishia kuwalaumu wasanii kwa kushindwa kuwa mfano kwa jamii inayowatazama

 Timu ya Blog hii imepokea picha zaidi ya 1000 za wasanii wa kitanzania na zipo katika hatua ya uhalili ili kupunguza ukali wa picha hizo kwa macho ya wapenzi wa blog hii. Picha nyingi zilizotumwa zimetumwa na watu wanaoshirikiana na wasanii hao kupiga picha hizo. Muda si mrefu zitaanza kuonekana kupitia Blog hii. Lengo la kufanya hivyo ni kufikisha ujumbe kwa jamii na waote wanaoiga mtindo huo madhara ya kupiga picha za ovyo na kushindwa kuzidhibiti
Jack wa Chuzi
Anaitwa Jack

Wema Sepetu

Aunt Lulu

Mary John

Afsa Kazinja

photo


photo

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua pazia kuzindua rasmi jengo la Kitivo cha Sayansi la Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro leo Machi 14, 2013 mjini Morogoro. Kushoto kwake ni Mkuu wa Chuo hicho Mama Mwantumu Malale.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo juu ya ujenzi wa jengo la kitivo cha Teknohama toka kwa Bw. Hamza Mustafa Njozi kabla ya kuzindua rasmi jengo la Kitivo cha Sayansi la Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro leo Machi 14, 2013 mjini Morogoro. Kushoto kwake ni Mkuu wa Chuo hicho Mama Mwantumu Malale.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipunga mkono kuaga wanafunzi na wafanyakazi baada ya kuzindua rasmi jengo la Kitivo cha Sayansi la Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro leo Machi 14, 2013 mjini Morogoro. Kushoto kwake ni Mkuu wa Chuo hicho Mama Mwantumu Malale.



photo





Jina lililotangazwa ni Jorge Bergoglio mwenye umri wa miaka 76 Papa mpya anatarajiwa kubariki umati uliokusanyika St. Peter's Square ambapo atakuwa akitambuliwa kwa jina la Papa Francis


photo

Wadau wakubwa wa blog hii, Advocate Berius Nyasebwa-Kushoto na Advocate Tundu Lisu ambaye pia ni Mbunge wa Singinda (Chadema) na Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni wakiwa katika picha ya pamoja.Taifa letu bado linahitaji vijana mawakili na wanasheria wa kutosha watakaoweza kusaidia jamii kubwa ya kitanzania ambayo kwa sehemu kubwa haifahamu haki na sheria mbalimbali zinazowalinda katika maisha yao ya kila siku.


Advocate Berious Nyasebwa akiwa katika pozi mara baada ya kuukwaa uwakili.

photo

Na Lydia Churi- MAELEZO
Serikali imewasimamisha kazi na itawafungulia mashtaka ya kijeshi Maafisa watano wa Jeshi la Polisi nchini kutokana na tuhuma mbalimbali za ukiukaji wa maadili na taratibu za jeshi hilo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Emmanuel Nchimbi (pichani kulia) amewataja waliosimamishwa kazi kuwa ni  Elias Mwita aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mbeya, Jacob Kiango aliyekuwa Msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mbeya na Charles Kinyongo aliyekuwa Mkuu wa kikosi cha kutuliza Ghasia Mkoa wa Mbeya.
Dkt. Nchimbi amesema leo jijini Dar es salaam kuwa  viongozi hao wamesimamishwa kazi tangu jana kutokana na kukiuka maadili ya jeshi la Polisi nchini ambapo wanatuhumiwa kwa madai kuwa walipeleka chumvi na sukari kwenye Ofisi ya Mkemia Mkuu badala ya kilo 1.9 ya madawa ya kulevya aina ya Cocaine yaliyokamatwa na askari mkoani Mbeya mwezi Machi mwaka jana.
Waziri Nchimbi alisema vitendo hivyo vinavyofanywa na viongozi wa jeshi la Polisi vinawavunja moyo na kuwapa hofu askari wa ngazi ya chini ambao hushindwa kufanya kazi zao kwa uadilifu unaotakiwa.  
Katika hatua nyingine, aliyekuwa mkuu wa Upelelezi mkoani Kagera Peter Matagi amesimamishwa kazi na atafunguliwa mashtaka ya kijeshi kutokana na kukiuka taratibu za kazi kwa kuwabambikiza kesi zisizo na dhamana wananchi 13 wa kata ya Nyakasimbi wilaya ya Karagwe mkoa wa Kagera Kutokana na vurugu za kugombea ardhi ambazo hazikuwiana na aina ya mashtaka walioshtakiwa hali inayoonesha dalili ya uwepo wa rushwa
Waziri Nchimbi alisema wananchi hao walibambikizwa kesi ya ujambazi wa kutumia silaha ambapo walikaa mahabusu kwa muda wa miezi miwili na baadaye timu ya uchunguzi iliyoongozwa na waziri mwenyewe kugundua kuwa mashtaka waliyoshtakiwa hayakuwa sahihi hali ambayo ilisababisha Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) aliifuta kesi.
Aidha, Serikali pia imemsimamisha kazi aliyekuwa Mkuu wa Polisi wilaya ya Serengeti Paul Mng’ong’o kwa kosa la kuingia katika Hifadhi ya Mbuga za wanyama ya Serengeti na kupanga njama ya kuchimba madini aina ya dhahabu ndani ya hifadhi hiyo hali iliyosababisha kiongozi huyo kushtakiwa  kwenye mahakama ya kiraia huko Serengeti.
Wakati huo huo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi aliyekuwa anasimamia ajira katika jeshi hilo nchini Renatus Chalamila amepewa likizo ya mwezi mmoja baada ya kutajwa mara nyingi kuhusika na kuwatoza fedha vijana walioomba ajira ya jeshi la polisi ili awapatie kazi hiyo.
Alisema Chalamila amepewa likizo hiyo na mapendekezo kupelekwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama mamlaka ya nidhamu  ili Rais afanye maamuzi juu ya tuhuma zinazomkabili askari huyo. 
Kufuatia hali hiyo jeshi la polisi limelazimika kuwaondoa katika mafunzo askari wanafunzi 95 waliokuwa wamejiunga na chuo cha polisi baada ya kubainika kuwa walipata fursa hiyo kwa kutoa fedha.
Waziri Nchimbi alitoa wito kuwa Serikali itawaunga mkono askari wanaofanya kazi kwa uadilifu ila watakaoenda kinyume na maadili na taratibu za jeshi la polisi serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria ikiwemo kuwafukuza kazi.
Hatua zilizochukuliwa na Serikali kwa viongozi wa jeshi la polisi ni sehemu ya makubaliano ya Maafisa waandamizi wa jeshi la Polisi nchini waliokutana hivi karibuni mjini Dodoma kulinda maadili ya jeshi hilo na kukabiliana na vitendo vyote vinavyolichafua jeshi hilo kwa jamii ili  kutatua kero za wananchi na kuzingatia utawala bora. 
SOURCE: MICHUZI JR

photo

Na Magreth Mgina
Jina lake halisi ni Latipher , si maarufu sana machoni pa watu lakini ni mahiri sana katika kazi, kama ulivyo mvuto wa umbile lake ndivyo alivyo na mvuto katika kazi ya sanaa ya uigizaji.

Kipaji chake kimedhihirika hivi karibuni baada ya kupata fursa ya kushiriki katika filamu ya Worl Of Benefit ambayo ipo katika hatua ya ‘editing’ ikisubiri kuingizwa sokoni.

Licha ya ushiriki wake wa ‘scene’ chache ndani ya filamu hiyo lakini Latipher ameweza kuonesha kipaji cha hali ya juu akiwa sambamaba na mkongwe Rose Ndauka.

Akizungumzia umakini wake katika kazi Latipher amesema hivi, “Awali, sikuwa na uzoefu mkubwa katika mambo ya uigizaji, lakini baada ya kukaa ‘camp’ kwa siku kadhaa na kupata mafunzo ya kutosha kutoka kwa wasanii wakongwe nilijikuta nikiingiwa na ujasiri, papo hapo nilianza kujituma na kufanya mazoezi bila kuchoka, nafurahi kuona nilichokipigania kimefanikiwa, nitaendelea kujifunza zaidi ya hapa ili baadae niwe muigizaji bora kabisa wa filamu.”

Washiriki wengine aliokutana nao Latipher katika filamu hiyo ni pampja na Mzee Chilo, Hemed Suleiman, Awadh Saleh, Mama Mjata, Timbulo, Peter, Tutti, Miriam na Natalia.


photo

 Baadhi ya machanguduoa wakipandishwa kwenye gari la polisi .


Baadhi ya machanguduoa wakipandishwa kwenye gari la polisi . katika Msako huo uliofanyika katika maeneo ya afrika sana mpaka mori sinza ilibainika pia kuwa baadhi ya wanaofanya biashara hiyo wengi wao ni wake za watu,wafanyakazi za ndani na wahudumu wa bar. Jumla machanguduoa 60 walikamatwa na kufikishwa katika kituo cha polisi usiku wa jumanne.

Zimetumwa na "Nginya the Blogger" kutoka Sinza Dar

photo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jayaka Mrisho Kikwete amemtumia salamu za pongezi nyingi Rais Mteule wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa Uhuru Kenyatta.

Katika salamu hizo zilizotumwa leo, Jumamosi, Machi 9, 2013, saa chache baada ya kuthibitishwa rasmi kuwa Mheshimiwa Kenyatta ameshinda Uchaguzi Mkuu wa Kenya uliofanyika mwanzoni mwa wiki hii Jumatatu, Machi 4, 2013, Rais Kikwete amemwambia Mheshimiwa Uhuru Kenyatta:

“Mpendwa Rais Mteule na Kaka, ilikuwa ni furaha kubwa kwangu kupokea taarifa ya ushindi wako wa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya. Niruhusu, kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Tanzania, na kwa hakika, kwa niaba yangu binafsi kukupogenza kwa dhati ya moyo wangu kwa mafanikio haya makubwa ya kuchaguliwa kwako.”

Ameongeza Rais Kikwete: “ Ushindi huu ni ushahidi na ishara ya wazi kabisa ya imani na matumaini ambayo wananchi wa Kenya waliyonayo katika uongozi wako. Huu ni utambuzi wa kazi yako maridadi na mchango wako mkubwa ambao umeutoa katika nafasi mbali mbali za uongozi katika siku za nyuma katika jitihada zako za kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii na ustawi wa nchi yako na wananchi wake.”

Amesisitiza Rais Kikwete: “Wakati unajiandaa kuchukua madaraka ya juu zaidi katika nchi yako, napenda kukuhakikishia msimamo wake binafsi pamoja na ule wa Serikali yangu wa kuunga mkono Serikali yako. Ni imani yangu kubwa kwamba pamoja tutaweza kuendelea kusukuma mbele zaidi maendeleo ya nchi zetu – Kenya na Tanzania na pia utengamano wa Afrika Mashariki kwa manufaa ya nchi zetu na wananchi wake.”

photo

Waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga
Muungano wa CORD wake Raila Odinga umeelezea kuwa unajianda kwenda mahakamani kupinga matokeo ya urais yaliyompa ushindi Uhuru Kenyatta.

Raila Odinga, amewaambia waandishi wa habari kuwa matokeo yaliyotolewa na tume hiyo yalikuwa yamehujumiwa hasa baada ya kutokea hitilafu katika mitambo ya elektroniki iliyokuwa inatumiwa katika shughuli hiyo.
Raila amedokeza kuwa muungano wao unajiandaa kwenda mahakamani kupinga matokeo hayo.

Aidha alisema kugoma kwa mitambo hiyo kulichanganya mambo katika shughuli ya kuhesabu kura. Alisema kuwa baada ya kutokea hitilafu, kura alizokuwa amepata katika maeneo bunge ambayo ni ngome zake , ziliongezwa kwa hesabu ya kura za muungano pinzani wa Jubilee.

Mapema wiki hii, wakati shughuli ya kuhesabu kura za urais ilikuwa inafanyika, CORD walielezea malalamishi kuhusu shughuli nzima hasa baada ya kura kuanza kuhesabiwa kwa mikono badala ya mashine.

Lakini mahakama kuu ilitupilia mbali kesi yao ikisema kuwa haina uwezo wa kufanya uamuzi katika kesi hiyo, na kuwa ni mahakama ya juu zaidi pakee inayoweza kusikiliza kesi hiyo.

photo

Nachukua fursa hii kuwapa maendeleo ya tiba ya Mwenyekiti wa TEF Absalom Kibanda ambaye amelazwa Hosipitali ya Millpark, Johannesburg nchini Afrika Kusini.
1. Kibanda leo ameingizwa theater ili kuanza kufanyiwa upasuaji na kujengwa sura baada ya kupungua kwa majeraha na uvimbe vilivyokuwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake, hususan kichwani na usoni.
2. Upasuaji huo unazingatia matokeo ya uchunguzi ulifanywa kwa zaidi ya saa 48 na jopo la madaktari na kubaini kwamba mbali na madhara ya awali, Kibanda pia aliumizwa taya lake la kushoto.
3. Kuhusu jicho lake la kushoto ambalo pia lilijeruhiwa, madaktari walisema wangetoa uamuzi kuhusu aina ya upasuaji ambao wangeufanya baada ya kubaini hali halisi wakati watakapokuwa wakijenga sura yake ambayo iliharibiwa kwa majeraha.
4. Wakati akipelekwa theater ambako alikuwa akifanyia upasuaji ambao uliotarajiwa kuchukua saa zaidi ya nne, alikuwa akilalamikia maumivu kutokana na kidonda kilichopo kwenye mguu wake wa kushoto. Kidonda hicho pia ni matokeo ya unyama aliyofayiwa.
5. Jana Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana ambao wako Afrika Kusini kikazi, walimtembelea Kibanda hosipitalini kumjulia hali. Rais Kikwete alisema Serikali inajitahidi kuwasaka wahusika wa tukio la utesaji wa Kibanda na kwamba wakikamatwa watafikishwa mahakamani.
Tutaendelea kufahamishana kila hatua ya tiba ya Mwenyekiti wetu, na tunaomba tuendelee kumwombea ili apone haraka.


--
Neville C. Meena,
Secretary General,
Tanzania Editors Forum - TEF,
Dar es Salaam - Tanzania.
Cell: +255 - 787 - 675555
+255 - 753 - 555556

photo


photo

Uhuru Muigai Kenyatta (born 26 October 1961) is a Kenyan politician who has served in the government of Kenya as Deputy Prime Minister since 2008. He is the Member of Parliament for Gatundu South Constituency and former Chairman of Kenya African National Union (KANU), which was a part of the Party of National Unity (PNU).

Kenyatta is the son of Jomo Kenyatta, Kenya's first president (1964–1978). His name, Uhuru, is Swahili for "freedom". He attended St Mary's Schoolin Nairobi. From there he went on to study political science at Amherst College in the United States.

Nominated to Parliament in 2001, he became Minister for Local Government under President Daniel arap Moi and, despite his political inexperience, was favored by President Moi as his successor; Kenyatta ran as KANU's candidate in the December 2002 presidential election, but lost to opposition candidate Mwai Kibaki by a large margin. He subsequently became Leader of the Opposition in Parliament. He backed Kibaki for re-election in theDecember 2007 presidential election and was named Minister of Local Government by Kibaki in January 2008, before becoming Deputy Prime Minister and Minister of Trade in April 2008 as part of a coalition government.

Subsequently Kenyatta was Minister of Finance from 2009 to 2012, while remaining Deputy Prime Minister. Accused by the International Criminal Court (ICC) of committing crimes against humanity in relation to the violent aftermath of the 2007 election, he resigned as Minister of Finance on 26 January 2012.

photo

Na Absalom Kibanda

HAKUNA shaka hata kidogo kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaugua maradhi mabaya kabisa ya uongozi ambayo yamekuwa yakikitafuna chama hicho kwa miaka mingi sasa.

Maradhi haya ya uongozi ambayo CCM inaugua hayakuanza leo na niseme wazi kabisa, hayakuanza wakati huu chama hicho kinapoongozwa na Rais Jakaya Kikwete ambaye ndiye mwenyekiti wake wa taifa.

Ushahidi wa kihistoria unaonyesha kwamba, maradhi hayo ambayo yamepewa majina tofauti na wachambuzi mbalimbali, yalianza kukitafuna chama hicho wakati kikiongozwa na mwenyekiti wake wa kwanza, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Kumbukumbu zinaonyesha kwamba, mara baada ya Nyerere kuamua kustaafu urais mwaka 1985 aliendelea kushikilia madaraka ya mwenyekiti wa CCM kwa takriban miaka mitano zaidi.

Wakati akichukua uamuzi huo, kwa makusudi na kwa kutambua haja ya CCM kujijenga, alifanya ziara nchi nzima akisema anafanya hivyo kwa makusudi mahususi ya kukiimarisha chama.

Ni wazi kwamba hatua ya Mwalimu na viongozi wenzake wa CCM wa wakati huo ilichangiwa kwa kiwango kikubwa na kubaini kwao kuwapo kwa nyufa na udhaifu wa kiuongozi ndani ya chama hicho.

Hata baada ya kufikia hatua ya kuamua kustaafu uenyekiti wa chama hicho na kumwachia aliyekuwa rais wa wakati huo, Ali Hassan Mwinyi, Baba wa Taifa kwa nyakati tofauti alipata kutoa kauli ambazo zilikuwa zikitoa mwelekeo wa wazi uliokuwa ukionyesha kuwapo kwa kasoro kadha wa kadha za kiuongozi ndani ya chama hicho.

Miongoni mwa kauli hizo ni pamoja na zile za kukifananisha chama hicho na kokoro ambalo hutumiwa na wavuvi kuvua samaki kwa namna kukusanya kila takataka na wakati mwingine kusababisha uharibifu mkubwa kwa viumbe vinavyoishi majini.

Si hilo tu, baadhi ya wana CCM wanakumbuka namna Mwalimu alivyofikia hatua ya kusema maneno mazito ambayo yamebandikwa katika kuta za vyumba vya mikutano na ofisi za viongozi wa chama hicho tawala; ‘‘Bila CCM Madhubuti Nchi Itayumba’’.

Kumbukumbu zinaonyesha kwamba, Baba wa Taifa alitamka maneno hayo wakati ule alipokuwa akikinyoshea kidole chama chake hicho hata kufikia hatua ya kukilaani, kukikea na hata kukaribia kabisa kukikana pale aliposema; “CCM si baba yangu wala mama yangu naweza kukihama”.

Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba, hofu, wasiwasi na mashaka yaliyopata kuonyeshwa kwa nyakati tofauti na Baba wa Taifa kuhusu CCM, chama alichokiasisi na akakipigania kwa moyo wake wote havijapata kutoweka au kutafutiwa tiba ya kudumu.

Maradhi ambayo Baba wa Taifa alipata kuyasema kuwa yanakitafuna chama hicho yameendelea kubakia kama yalivyo na kwa bahati mbaya zaidi mengi kama si yote yamezidi kuota mizizi na kustawi.

Ni kwa sababu ya maradhi hayo ambayo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameyafananisha na saratani ya damu iliyosambaa katika mishipa, CCM imekuja na dhana mpya ya kujivua gamba iliyovuta hisia zenye ukinzani mkali wa hoja kutoka kwa wachambuzi tofauti wa masuala ya kisiasa.

Katika kuonyesha namna maradhi hayo yalivyokitafuna na yanavyoendelea kukidhoofisha chama hicho kwa kiwango cha kuwatia hofu viongozi wake, Rais Kikwete akaja na msamiati huo mpya.

Ili kuweza kujibu maswali ya wadadisi wa mambo wanaoisuta CCM wakisema inakabiliwa na tatizo kubwa la ombwe la uongozi, Kikwete akatumia mamlaka aliyopewa kuunda tume iliyojumuisha jopo la wataalam na wanazuoni wenye mapenzi mema na chama hicho.

Tume hiyo iliyojumuisha maprofesa na madaktari wa falsafa ikaongozwa na Wilson Mukama ambaye matokeo ya kazi waliyoifanya kwa muda wa wiki mbili kwa kujifungia katika hoteli moja kubwa ya nyota kadhaa yakamfanya ajikute akiukwaa ukatibu mkuu wa chama hicho.
Matukio haya yote ni kielelezo cha wazi kwamba, maradhi yale yale ya uongozi ambayo yamekuwa yakikitesa chama hicho kwa miaka nenda, miaka rudi yameendelea kukitafuna pasipo kukoma.

Pasipo kujua au pengine kwa mhemuko wa madaraka, Kikwete ambaye ndiye mwenyekiti wa taifa wa chama hicho akajitwika mzigo mzito wa kuongoza harakati za kukinusuru chama chake.
Huku akijua kuwa chama hicho kimelelewa katika misingi ya ‘zidumu fikra za mwenyekiti’ akajitwisha wajibu wa peke yake wa kuunda tume na kisha ili kuweza kukidhi utashi wake binafsi akajenga hoja ya kuwalazimisha wajumbe sekretarieti na wale wa kuchaguliwa wa kamati kuu kujiuzulu.

Yaliyofuata baada ya hapo sote tunayajua. Sekretarieti mpya ikaundwa huku nyuma na kwa siri ikibeba ajenda ya kuwalenga watu fulani fulani na wakati mwingine kupoza hasira za baadhi ya watu ambao angeweza kupata wakati mgumu kuwatupa kwa namna jongoo atupwavyo na mti wake.

Kinara katika sekretarieti mpya akawa Mukama, mtu ambaye tume yake ilibeba ajenda ya kuwashughulikia watu ambao tangu Kikwete aingie madarakani wamejikuta wakipita katika karai la moto kinyume kabisa na matarajio makubwa waliyokuwa nayo miaka sita tu iliyopita.

Kwa namna ile ile ilivyofanya kazi Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Dk. Harrison Mwakyembe miaka minne iliyopita, tume ya Mukama nayo ikawalenga watu wale wale na sababu zikiwa ni zile zile: Ufisadi.

Jasiri haachi asili. Kikwete yule yule aliyepata kuwanyoshea kidole ‘marafiki’ zake akisema kwamba urais wake hauna ubia, akakunjua makucha ya mamlaka safari hii akielekeza mashambulizi kwa kundi la watu wale wale ambao miaka kadhaa tu iliyopita walikuwa sambamba katika harakati za kusaka madaraka.

Baadhi yetu hatukupata shida kuelewa ni kitu gani kilikuwa kikitokea wakati tulipowasikia viongozi wapya wa CCM, Naibu Katibu Mkuu (Tanzania Bara), John Chiligati na Katibu wa Idara ya Uenezi na Itikadi, Nape Nnauye wakitangaza kile walichokiita Maazimio ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM.

Taarifa ambazo zilivuja miongoni mwetu hata kabla ya kuanza kwa kikao hicho cha NEC, zilikuwa zikieleza bayana kwamba, wembe ulikuwa ni kuwang’oa fulani na fulani ndani ya CCM.

Hatukuwa na sababu ya kuuliza sababu za maamuzi hayo kuchukuliwa kwani sote tulijua fika kwamba, makusudi makubwa ya maamuzi hayo yalikuwa ni kinyang’anyiro cha urais cha mwaka 2015.

Watu tunaoufahamu utamaduni wa CCM wa kuhujumiana kisiasa na kulana wenyewe kwa wenyewe kama njia ya kupata madaraka katika taifa hili tukakumbushwa masahibu yaliyopata kuwakuta wanasiasa wa aina ya John Malecela, Frederick Sumaye, Dk. Salim Ahmed Salim na Iddi Simba wakati wa mchakato wa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.

Kwa sababu hiyo basi, tuliposikia walengwa wa safari hii wakiwa ni watatu tu, miongoni mwao wakiwa ni wale walioratibu ajenda za kuwamaliza wenzao mwaka 2005, tukaona tunao wajibu wa kuwaeleza wasomaji wetu kile ambacho kilikuwa kikiendelea ndani ya chama hicho tawala.

Wakati tukijifanya kidomodomo kuusema ukweli huo mchungu, tukasahau ukweli kwamba nyuma ya ajenda hii ya leo, wako vinara wawili ambao ndiyo waliokuwa wapishi wakuu wa majungu yaliyowamaliza akina Salim, Simba, Sumaye na Malecela.

Jambo baya zaidi, nyuma ya karata yetu hii ya kujifanya tukiwa vimbelembele kusimamia na kuutetea ukweli huu ulio bayana, tukajifanya tukiipuuza nguvu kubwa waliyonayo vinara wa mkakati huo ambao kinara wao ndiye mkuu wa kaya aliyeshika mpini wakati sisi tukiwa tumekamata makali.

Ukweli kwamba wapishi wa ajenda hii walikuwa na timu kubwa ya makachero walio serikalini na walio idarani ukawa silaha kubwa ya kutujeruhi, baadhi yetu vibaya sana.

Huku wakijua kwamba tulikuwa tumeshang’amua janja yao ya kutafunana wenyewe kwa wenyewe kwa gharama za kufifisha turufu muhimu ya ushindi wa demokrasia ya vyama vingi iliyoanza kuchanua katika uchaguzi mkuu uliopita, makachero hao wa CCM na mawakala wao walio serikalini, wakaja na uzushi ule wa siku zote.

Kwa ustadi mkubwa huku wakitumia uzoefu wao wa kupindisha mambo, makachero hao wakafanikiwa kupenya katika mioyo ya baadhi ya viongozi wa kidini na wale wa vyama vya siasa vya upinzani ambao wakajikuta wakishangilia dhana isiyo na mashiko ya CCM kujivua gamba.

Walipoona hilo halitoshi, wakarejea ndani ya vyumba vyetu vya habari na wakatumia udhaifu wetu wa kufikiri sawasawa kutulisha uzushi wao wakituaminisha kuwa ni wa kweli ukielekezwa kwanza miongoni mwetu na kisha miongoni mwa walengwa wakuu wa ajenda nzima ya kujivua gamba.

Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba, makachero hao wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa kulihadaa taifa kupitia vyombo vyetu vya habari na wakati mwingine kwa kuwatumia viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani ambao hawajui kuwa ile dhana ya zidumu fikra sahihi za mwenyekiti (wa CCM) imeshapenya ndani ya mioyo yao.

Ni jambo la kukatisha sana tamaa kwamba, japokuwa sote kwa ujumla wetu tunatambua vyema kuwa ajenda nzima ya kujivua gamba iliyoasisiwa na mwenyekiti wa taifa wa CCM ina harufu ya dhuluma, uonevu, kupakana matope na kuua ustawi wa mfumo wa vyama vingi bado tumeendelea kushangilia maamuzi hayo.

Matokeo yake makosa yetu hayo yamesababisha wanahabari tujikute tukiwa mavuvuzela wa ajenda ya kujivua gamba, tukipaza sauti na kuimwagia sifa lukuki pasipo kujua kwamba tunafanya hivyo kwa gharama za ustawi wetu wenyewe wa sasa na wa siku zijazo.
Hitimisho la yote hayo linatufanya sote kama taifa, kwa kujua au kutojua tujikute tukiwa majeruhi wa dhana iliyopitwa na wakati ya zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM pasipo kujali usahihi, malengo, makusudi na mwelekeo mzima wa kifalsafa wa fikra hizo. Hatupaswi kwenda huko.

photo


Mwanvita Makamba, akiwa katika chumba alicholazwa Mhariri Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd, Absalom Kibanda, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri wakati alipomtembelea kumjulia hali katika Hospitali ya Milpark baada ya kufikishwa katika hospitali hiyo jana usiku nchini Afrika ya Kusini.

photo



WANACHAMA wa timu kubwa za Simba na Yanga wa mkoani hapa wamepokea kwa furaha uamuzi wa viongozi wawili wa Simba kujiuzulu nyazifa zao kwa sababu mbali mbali zikiwemo za mabingwa hao wa Tanzania bara kufanya vibaya kwenye ligi kuu ya Tanzania bara na ligi ya mabingwa Afrika.
Kufuatia hali hiyo baadhi ya wanachama wa timu hizo waliohojiwa kwa nyakati tofauti na Mtandao huu leo asubuhi walidai kwamba hatua hiyo huenda ukaondoa jinamizi la timu hiyo kufanya vibaya,wakidai kwamba viongozi wa timu hiyo ndio chanzo cha timu hiyo kufanya vibaya hivyo.
Takribani mwenzi mmoja sasa baadhi ya wanachama wa timu hiyo kote nchini walishinikiza viongozi wote wa timu hiyo kujiuzulu kwa madai kwamba wao ndio chanzo cha timu yao kufanya vibaya, miongoni mwa wanachama waliolipotiwa kushinikiza viongozi hao kujiuzulu ni wanachama wa tawi lenye nguvu la Mpira Pesa mabpo baada ya tawi hilo  kushinikiza jambo hilo uongozi wa timu hiyo ulilipiga mkwara na baadae kutangaza kulifungia.
Baada ya kuona kelele zinazidi jana viongozi wawili wa timu hiyo makamu mwenyekiti Godfrey Nyange'Kaburu' na mwenyekiti wa kamati ya usajiri Zacharia Hans Pope walitangaza kujiuzuru nyazifa zao hizo kwa maandishi.
Kufuatia uamuzi huo wa kijasili uliofanywa na  viongozi hao wawili  wanachama wa yanga na simba mkoani hapa wamewaponmgeza viongozi hao kwa hayua yao yab kuweka maslai ya timu mbele huku wakiwaponda wiongzo wanaoendela kung'angania madaraka kwenye timu hiyo.
" Rage alikaririwa na redio moja akisema kwamba kufanya vibaya kwa Simba uongozi hauusiki,wahusika ni wachezaji na benchi la ufundi mimi ni mwanachma wa yanga laniki nasema kauli ile ya Rage ni ya kizushi,mfano mimi ni dereva wa hii taksi mtu kagonga gari langu  kwambele nakulihabirbu vibaya muhusika kanilipa pesa nyingi sasa mimi badala ya kununua taa za mbele nakwenda kununua taa za nyuma tena zinmgine haziwaki, pointi yangu ni kwamba uongzi wa Simba umeuza kwa pesa nyingi washambuliaji wawili Mbwana Samata na Emmanuel Okwi,badala ya pesa hile kununua wahsmbuliaji wao wamenunua kipa ambapo hitaji la Simba lilikuwa sio kwenye nafasi ya kipa Kaseja bado anauwezo,hivyo kumnunu kipa wa Uganda ambaye ni mgonjwa ni sana na kununua taa za nyuma ambazo haziwaki hivyo Rage kusema hausiki mimi na kataa"alisema Salum ambaye ni mwanachama wa yanga

Naye Bernard alipohojiwa alidai kwamba timu yao ya simba tatizo liko kwenye uongozi na kwamba binafsi anawapongeza sana Kaburu na Hans Pope kwa kuweka maslai ya klabu mbele kwa kujiuzulu kwa lengo la kuepusha migogoro isiyokuwa na tija kwenye timu yao.
" Rage anachong'angania ni kitu gani au hizo pesa za Okwi?  kumbukumbu zinanionyesha hali kama hii iliwakuta watani zetu yanga viongozi wote walitangaza kujiuzulu Nchunga peke yake aligoma kufanya hivyo mpaka alivyotishiwa kuvamiwa nyumbani kwake ndio akatangaza kujiuzulu kwa shingo upande hayo ndio anayotaka Rage "alisema

photo


photo

Tunajifunza nini kutokana na bango hili?

photo


Wadau wa blog hii Hemed na Awadh wakiwa katika pozi baada ya team ya blog hii kuwatembelea katika location inapotayarishwa movie yao mpya ya WORLD OF BENEFIT. Movie hiyo iliyosheheni vipaji na mastaa wakubwa ipo katika hatua za mwisho.

Picha kwa hisani ya Mcddenis Mgatha

photo



Hii ndio hali halisi ya Hospitali ya mkoa wa Morogoro. Wagonjwa wanalazwa sakafuni, Stand za Drip hakuna, wauguzi hawana gloves za kuvaa mikononi. Huu ni ujumbe kwa mbunge wa Morogoro Mjini bwana Abdul Aziz Abood ambaye kwa muda mrefu sasa amekuwa akitoa misaada ya magari ya kuzikia pindi watu wanapofariki badala ya kuangalia njia nyingine mbadala ya kusaidia jamiihasa katika huduma za afya.

Msaada wa magari ya kuzikia watu waliokufa si sehemu ya huduma ya afya

photo