Huyu ndiye Miss Tanzania wa kwanza kabisa ambaye kaka michuzi ametupatia taarifa za hivi karibuni kuwa hatuko naye tena duniani....alikuwa akijulikana kwa jina la mama theresa. kwa habari zaidi bofya hapa

Sio siri...habari hizi zimenishtua sana...asanate sana kaka michuzi kwa taarifa hii muhimu


Mwinjilisti wa kimataifa Amon Mkangara..kwa habari zake zaidi hebu bofya hapa.


Hawa ni moja kati ya watoto wengi waliotoka kufanyiwa.....kwa habari zaidi bofya hapa www.saharanvibe


Hili ni ziwa masoko..ni moja kati ya maziwa machache yenye maajabu na historia ya pekee kama ile ya Ziwa kisiba....watu mbalimbali hufika kuangalia mandhari ya ziwa hili lililozungukwa na milima.



Hapa ndipo yalipokuwa makao makuu ya serikali ya kikoloni ya wajerumani...
Majjid Mjengwa niambie hapa ni wapi?


Nyumba nyingi kijijini kwetu huonekana hivi.Hapa ni Tukuyu...wilaya ya Rungwe


Mashamba ya chai
Mlima Rungwe unavyoonekana kwa mbali
Wanajiografia nisaidieni....hii inaitwa nini vile?


Hili ndilo daraja laMungu lililoko mbele kidogo ya Kiwira.Hapo zamani daraja hili lilikuwa na maajabu ya pekee.Siwezi kueleza maajabu yote lakini hiko kidaraja unachokiona hapo hakijawahi kujaa hata siku moja hata mafuriko yawe makubwa kiasi gani...
Haya ndiyo maporomoko ya Kaporogwe...kwa kidhungu wanasema ..Kaporogwe falls
Mto Kiwira


Hivi karibuni nimepata maoni kupitia email na namba yangu ya simu kutoka kwa wadau mbalimbali wa blog hii kuwa wanapata shida sana katika taratibu za kutuma maoni yao.
Zifuatazo ni hatua muhimu katika kutuma maoni kupitia blog hii


1. Bofya kwenye sehemu iliyoandikwa maoni

2. ikishafunguka bofya tena sehemu iliyoandikwa post a comment

3.Ikifunguka anza kuandika maoni yako

4.Jaza maneno yanayoonekana katika kiboksi (word verification) kisha

5.Chagua sehemu iliyoandikwa anonymous kisha

6.Bofya sehemu iliyoandikwa "publish your comment "
Ukikamilisha taratibu hizi hapo maoni yako yatachapishwa moja kwa moja katika sehemu ya maoni.


Karibu tena....




Mtangazaji wa radio ya watu...Tayana


Hapa nimepozi na mdau wangu

photo





Hapa ni uwanja wa mpira sokoine ambapo wanaume halisi walifanya makamuzi ya kufa mtu.Afande sele anaonekana kwa mbali akiwapag....mashabiki
Mashabiki


Rais Joseph kabila siku alipofunga pingu za maisha...kaka michuzi umeiona hii?jina siwatajii..ila atakayelipatia nitampa zawadi




Magari mbalimbali yakielekea eneo la chuo kikuu Dar kwa ajili ya kubeba mizigo ya wanafunzi.
Picha na Issa Michuzi.

photo

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam wakifungasha vilago baada ya kutolewa kwa tamko la kuondoka chuoni hapo baada ya mgomo wa kuingia darasani ili kuishinikiza serikali kutoa asilimia 100 kkwa hela ya field.

photo

Mwanamuziki Ray C katika katika pozi
Salama Jabri...mtangazaji wa Kituo cha East Africa radio na Tv,mwana Dada huyo ni mmoja kati ya wadau wakubwa wa maendeleo ya muziki wa bongo fleva hapa nchini.
Jacline.......siku hizi amekuwa mwanamuziki wa......

photo

Mchungaji Mtani...ambaye ni askofu wa kanisa la waadventista wasabato nyanda za juu kusini.

photo

Mandhari ya chuo cha ufundi veta-mbeya yanavyoonekana

Huku ughaibuni kila kitu mmea unaouna ni kijani tu

photo

Kuna mdau ameniomba nimtumie picha zinazoonesha sura ya jiji la Mbeya kupitia Blog hii.
Hapa ni sehemu ya mnara kama unaelekea Hospitali ya taifa ya Rufaa Mbeya
Kwa mbali ni round about kama unashuka kwenda stend kuu ya mabasi Mbeya
Safu za milima ya mbeya zikionekana kwa mbali

Stendi kuu ya mabasi mbeya inavyoonekana kwa mbali

photo

Jinsi soko la Mwanjelwa lilivyoungua
Baadhi ya watu wakishuhudia jinsi moto ulivyolitafuna soko la mwanjelwa huku wengine wakijaribu bahati zao kwa kufukuafukua hapa na pale.

photo

Siku soko la mwanjelwa lilipokumbwa na zahama ya moto..kama ilivyo kawaida yetu...matukio ya hatari kama haya yanapotokea huwa hatubaki nyuma katika kushuhudia...ingawa ilikuwa ni usiku lakini watu kibao kutoka pande mbalimbali za jiji la mbeya walikusanyika kama unavyowaona hapa

photo

Remigius Komba a.k.a Reyme K -Chief photographer wa Blog hii akiwaza kwa makini jinsi ya kuweza kuiboresha zaidi blog hii kwa picha zenye ubora na kiwango cha hali ya juu.Mshikaji ni mwanafunzi wa mwaka wa pili Digrii ya sheria chuo kikuu Mzumbe.
Sio siri jamaa anatisha sana katika maswala ya photos...michuzi upo?ana ma skilz kibao katika maswala ya production za muziki,picha na kompyuta.
Kwa taarifa yako...picha zote unazoziona humu ni kazi ya mikono yake Reyme K.


MDAU

1 Comment Imetumwa na Unknown at 4/01/2007 04:38:00 PM

Upendo Merere a.k.a-Perlon mmoja wa wadau wakubwa wa Blog hii akiwa katika pozi wakati akitoka katika kikao cha wanafunzi watokao mikoa ya nyanda za juu kusini kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo kikuu Mzumbe-Mbeya Campus.

photo