Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Mfalme Mswati wa (ii) wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. Mfalme Mswati wa ii, ametua nchini kwa ajili ya
kuhudhuria Mkutano wa 'Smat Patnership' unaotarajia kuanza Juni 28 mwaka huu. Source: www.wazalendo25.blogspot.com

photo ,

Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini wameitaka Serikali kutumia njia ya mazungumzo kumaliza migogoro, badala ya kutumia jazba na nguvu.

Vilevile, wamesema kuwa hawako tayari kukaa kimya huku wakiona amani na utulivu nchini ikivurugika, badala yake wataendelea kusema ili amani na utulivu viweze kurejea.

Kauli hiyo imekuja baada ya Rais Jakaya Kikwete, kuwataka maaskofu hao na viongozi wengine wa dini nchini kuendelea kuisaidia Serikali katika kuimarisha amani na upendo miongoni mwa wananchi.

Akizungumza wakati wa kuadhimisha Jubilee ya miaka 25 ya uaskofu wake kwenye sherehe zilizofanyika jana katika Seminari ya Mt Peter mjini Morogoro, Askofu wa Jimbo la Morogoro, Telesphor Mkude, alisema meza ya mazungumzo ni lazima itumike katika kuimalisha amani na upendo wa Watanzania badala ya kutumia jazba na nguvu.

Mkude alisema kwa hivi sasa kumeibuka mivutano ya kidini na kisiasa na kutoa mfano wa vurugu zilizoibuka wilayani Sengerema mkoani Mwanza juu ya nani ana haki ya kuchinja au kutokuchinja kati ya waumini wa madhehebu ya Kikristo na Waislamu.

Pia vurugu za mikutano ya kisiasa, makanisa kuchomwa, mapadri na watumishi wengine kuuawa na kuteswa, kutupwa kwa mabomu katika mikusanyiko ya watu ikiwamo makanisa na kwamba yote hayo yangeweza kumalizwa katika meza ya mazungumzo.

Vurugu kubwa zilitokea Jumamosi iliyopita mjini Arusha baada ya mtu ambaye bado hajajulikana, kutupa bomu katika mkutano wa Chadema wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika katika viwanja vya Soweto na kuua watu wawili na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa.

Mei 2, mwaka jana, Mwandishi wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daud Mwangosi aliuawa kwa kulipuliwa na bomu na askari polisi katika vurugu zilizotokea katika eneo la Nyololo mkoani Iringa.

Februaria 18, mwaka huu, Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Minara Miwili, Mji Mkongwe, Zanzibar aliuawa kwa kupigwa risasi asubuhi wakati akienda kuendesha misa katika Kanisa la Mtakatifu Theresia eneo la Mtoni. Mtuhumiwa wa tukio hilo, Omar Musa Makame, anaendelea na kesi mahakamani kujibu tuhuma za mauaji.

Tukio lingine ni lile la watu wawili kuuawa na polisi mjini Songea, Februari 22, mwaka jana, wakati wakizuia maandamano ya wananchi wenye hasira kali waliokuwa wakipinga mauaji yanayohusishwa na imani za kishirikiana.

Hivi karibuni maaskofu hao walitoa tamko la kuitahadharisha Serikali, kudhibiti vurugu za kidini na kisiasa nchini.

Walionya kuwa iwapo vurugu hizo hazitadhibitiwa huenda nchi ikaingia katika machafuko.Awali, jana Rais Kikwete akizungumza katika hafla hiyo licha ya kumpongeza Askofu Mkude kwa utumishi wake mwema wa miaka 25 ya uaskofu wake, lakini pia alimpongeza kwa kuwa na mchango katika jitihada za maendeleo zinazofanywa na Serikali.
Alisema Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro limekuwa msaada katika kuimarisha huduma za jamii ikiwamo sekta ya elimu na afya na kwamba baadhi ya zahanati na vituo vya afya vimejengwa na kupandishwa hadhi kama Hospitali ya Mt Kizito na Turiani.

Rais Kikwete aliongeza kuwa mbali ya askofu huyo kuisaidia Serikali katika nyanja hizo, pia amekuwa akiiunga mkono katika jitihada zake za kujenga amani na upendo miongoni mwa wananchi ili taifa liweze kuwa na raia wema.

Kwa upande wake Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, alimtaja Askofu Mkude kuwa ni kuhani asiyekuwa na mwanzo wala mwisho, kwa vile anashiriki katika ukuhani wa Yesu Kristo asiyekuwa na mwanzo wala mwisho.

Alisema mpaka kufikia umri huo katika utumishi wake amekutana na mambo mengi magumu, lakini kutokana na kumtegemea Mungu zaidi ameshinda na kwamba akawaomba waumini wa Kanisa Katoliki kuendelea kumwombea na kumpa ushirikiano ikiwa ni zawadi yao pekee .

Askofu Mkude aliteuliwa kuliongoza Jimbo Katoliki la Tanga mwaka 1988 na aliyekuwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Paulo II (kwa sasa ni marehemu), mwenye heri na miaka mitano baadaye alihamishiwa katika Jimbo la Morogoro ambako amelitumikia kwa miaka 20 mpaka sasa

photo

UONGOZI WA BLOG HII UMEPATA NAKALA YA MKANDA WA VIDEO UNAOONYESHA TUKIO ZIMA LA NAMNA MLIPUKO WA BOMU KATIKA MKUTANO WA CHADEMA ULIVYOTOKEA. UONGOZI WA BLOG  UNAWASILIANA NA WANASHERIA KUONA KAMA VIDEO HIYO INAWEZA KUBANDIKWA KATIKA BLOG HII. TUTAWAJUZA SOON

photo

Katika  hali  yakushangaza , mbunge  wa  mbeya  mjini  kwa  tiketi  ya  CHADEMA, mh.  SUGU  ameporomosha  tusi  zito  kwa  waziri  mkuu  wa  tanzania  ( mh. PINDA )  akidai  kuwa  Tanzania  haijawahi  kuwa  na  waziri mkuu   mpumbavu  kama  yeye.....

Tusi  la  Sugu  limekuja  baada  ya waziri  mkuu  kuwaruhusu  rasimi  polisi  kutumia  nguvu  ya  ziada   kuwadhibiti  wananchi  kwa  kuwashushia  kichapo  ili  wazitii  sheria.....

photo

Baada ya mh.waziri mkuu mizengo pinda kutoa ruhusa kwa polisi kupiga wananchi..Mh mbunge zitto kabwe nae atoa lake juu ya mh.waziri mkuu...Kupitia tweet yake Zitto alisema "Viongozi wa kisiasa lazima wajue kuweka akiba ya maneno yao ,kuropoka hovyo hovyo wakati kama huu wenye taharuki ni hatari sana"..Aliongezea "Ni lazima viongozi wawajibishwe kwa maneno wanayotamka.Mh. Pinda anahamasisha ukiukwaji wa katiba na sheria Asipowajibishwa.!"

photo

Taarifa ambazo zimepatikana kwenye mitandao ya Ki-jamii zinaelezwa kuwa, jana usiku katika kata ya Minepa jimbo la Ulanga Magharibi, vijana waliosadikiwa kuwa wa “green guard” waliwavamia viongozi wa CHADEMA na kuwajeruhi...

Waliojeruhiwa ni Mwenyekiti wa Jimbo bw. Kibam Ally Mohammed (aliyevaa shati ya michirizi), Katibu wa Jimbo bw. Lucas Lihambalimo (aliyevaa shati jekundu) na Bw. Severin Matanila, Katibu Mwenezi tawi la Minepa (aliyekaa, mwenye bandeji), ndiye mlinzi wa mgombea.

photo

KIPANDE CHA VIDEO KIKIOYESHA NAMNA MLIPUKO ULIVYOTOKEA
Kutoka kushoto mwenye Fulana Nyekundu ameumia vibaya sana, mtu wa pili kwake ni mwanadada Judy ambaye alipoteza maisha palepale. aliyeshika laptop ni mwana jamii forum
.

Baadhi ya Watoto waliokaa hapo juu ndiyo waliokufa na baadhi kuumia vibaya kwa bomu, hapo ndipo bomu lilipo angukia..

photo


DSC09341Mwenyekiti wa Chadema, Mh freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini Mh. Godbless Lema wakiwa katika uwanja wa Soweto, wakati wa zoezi la kuchukua vipimo mbalimbali chini ya usimamizi wa wataalamu toka Jeshini.
DSC09327
Mhe.Mbowe na Mhe. Lema wakishauriana jambo..
DSC09343Eneo la maafa. Inaelezwa kuwa wataalamu wa jeshi waligundua kuwako kwa kitu ndani ya tanki la mafuta na hivyo kuamua kulikata. Taarifa hizo zinadai kwamba kulikuwa na mabomu yametegwa chini ya gari na hivyo tank hilo lilishamabuliwa kwa risasi labda utokee mlipuko! Pia gari la matangazo lina majeraha mawili katika mlango wa kushoto yaliyotokana na kitu chenye ncha ambacho kinaweza kuwa risasi au vipande vya vyuma vya bomu.
DSC07458
Gari ambalo linasadikiwa kutegwa bomu katika tanki la Mafuta.

DSC09360Mh. Mbowe akiwa nyumbani kwa wazazi wa mmoja wa marehemu (Ramadhani) eneo la Mianzini kuwapa pole kwa kuondokewa na mpendwa wao.
DSC09382James Ole Millya na Mbunge Lema wakimjulia hali mmoja wa majeruhi walilazwa katika hospitali ya Seliani Jijini, Arusha.
DSC09373Mtoto Sharifa nae amelazwa hospitalini hapo kwa majeraha ya mlipuko katika hospitali ya Seliani Jijini, Arusha.
DSC09377Dereva wa mgombea wa Chadema Kata ya Themi, Bw beni akiwa majeruhi kitandani,katika hospitali ya Seliani Jijini, Arusha.Habari hii kwa hisani ya Wazalendo 25 Blog

photo , ,








photo



MAELEZO YA MASHUHUDA
  • Bomu lililolipuka limejeruhi watu sana. Inaonekana bomu lilitegwa karibu na gari la matangazo.
  • Mtoto aliyelipukiwa na bomu amefariki uwanjani.
  • kijana mdogo kabisa ameuwawa. Ana tundu sehemu ya kifuani kushoto. Kwenye moyo. Inadhaniwa ni risasi. Hospitalini Mount Meru wanasema wamempokea akiwa amekufa tayari.
    • Kijana mwingine mdogo amejeruhiwa sana kichwani, kiasi kwamba ubongo unatoka yuko Mount Meru. Watu walioumia ni wengi sana sana. Mwenyekiti Mbowe amekwenda Selian Hospitali na Mount Meru Hospital na sasa pamoja na Lema wako eneo la tukio.

photo

Mgambo wa jiji la Dar es Salaam wakiwa katika zoezi la kuwakamata Madada wanaofanya biashara ya kuuza miili yao wajulikanao kama Machangudoa katika eneo la Sinza. Picha mbalimbali zikionyesha namna walivyokuwa wakipakiwa ndani ya Gari tayari kwa kupelekwa katika vyombo vya sheria



photo

Basi la kampuni ya ABOOD BUS likiwa limepinduka  katika eneo la mkambarani siku ya jumatano alfajili ya saa kumi na moja na kujeruhi watu na kukimbizwa hospitali ya mkoa wa Morogoro, hakuna mtu aliepoteza maisha katika ajali hiyo.

photo




Mama mzazi wa marehemu Albert Mangweha akiwa ameshikilia tuzo aliyopewa kwa niaba ya mwanae, tuzo hii aliipata msanii Kala Jeremiah kwenye tuzo za Kilimanjaro ikiwa kama tuzo ya msanii bora ya Hip Hop 2013-14

photo


Mwanasheria Mshauri na Mtetezi wa Haki za Binadamu Mkoani Morogoro ambaye pia ni Mwasisi wa Blog hii Amani Mwaipaja anatarajia kuzindua vitabu vyake viwili katikati ya mwezi wa Saba. Vitabu Vitakavyozinduliwa ni pamoja na IJUE SHERIA NA HAKI ZAKO na kitabu cha UKWELI USIOPENDWA.

Kwa mujibu wa Mratibu wa tukio hilo-Felista Lyamba, tarehe rasmi ya Uzinduzi itatajwa hapo baadaye. Ifuatayo ni sehemu fupi ya utangulizi wa kitabu cha Ukweli Usiopendwa


Taifa Linaangamia

Tumo katika taifa lililogubikwa na maswali. Watu hawaoni tena nuru kwa maisha yao ya baadae. Mazungumzo ya watu barabarani, kwenye vyombo vya usafiri, vyombo vya habari, maofisini, sehemu za ibada, vijiweni na kwenye mikusanyiko ya watu hujiuliza tunakwenda wapi. Ugumu wa maisha umewafanya wengine wazikimbie familia zao huku wengine kwa kuchanganyikiwa wamejiua na kuua wenzao.

Maisha ya wengi yamekuwa ya kubahatisha na kukata tamaa. Hali ya kukata tamaa iliyoenea miongoni mwa wananchi wengi haitokani tu na matatizo peke yake wala maovu katika jamii. Kinachokatisha tamaa zaidi ni kuona viongozi wao walioapa kuwalinda dhidi ya uovu wakicheka na uovu wenyewe na wakati mwingine wanakumbatiana na waovu hadharani. Mpaka sasa hakuna dalili kwa viongozi kumaliza kucheka

Serikali sasa inakabiliwa na changamoto nyingi kutoka kila upande. Ni kama mfumo mzima wa utawala umesimama na Mungu ndiye ajuaye nini kitatokea kesho na keshokutwa ndani ya taifa letu.  Nchi inakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira, umasikini uliokithiri, rushwa hususan kwenye mikataba ya kinyonyaji inayowanufaisha watu wachache katikati ya mamilioni ya watanzania. Uporaji wa rasilimali za taifa, mishahara midogo isiyoendana na hali ya maisha, kuporomoka kwa uchumi na huduma mbovu za kijamii ni baadhi tu ya dalili za ugonjwa hatari uliolikumba taifa.

Ugonjwa huo umetengeneza matabaka ndani ya taifa moja ndio maana mara kadhaa wanazuoni, wanasiasa na wananchi wamekuwa wakilalamika na kutaka mabadiliko ya kulikwamua taifa kutoka hapa lilipo. Ama kwa hakika taifa linaugua, linaugua ugonjwa wa ajabu.

Serikali, licha ya kuwa na nguvu kubwa ikitumia polisi, magereza, jeshi la wananchi, usalama wa taifa na wataalam waliobobea kwenye kila fani nayo imeshindwa kuwabana wabadhilifu ambao ndio virusi vya ugonjwa huo. Wanafanya wapendavyo bila kujali shida za watu wengine wakiwa chini ya mwamvuri wa chama cha mashetani

Ufisadi unazungumzwa kila mahali, nani asiyepata kusikia habari zake?, vipofu, ingawa hawaoni lakini maisha wanayoishi na yale wanayoyasikia yanatosha kuwashuhudia hali ya taifa letu. Bubu, ingawa hawezi kusema na kusikia lakini anayoyaona ni sauti za ajabu zinazopenya mpaka katika mawazo yake ya ndani.

Mahakimu wamepotoka, wanahongwa kwa rushwa na kudanganywa. Ulevi, fujo, kukosa uaminifu wa kila namna kumeshamiri miongoni mwa wale wanaozisimamia sheria. Hivi sasa, kwasababu chama cha mashetani hakiwezi kuudhibiti ukweli unaowekwa wazi na wazalendo kila kukicha, sasa kinaendeleza mbinu ya kuwagawa watanzania kwa dini, rangi, ukabila na hata jinsia. Watawala wanasukumwa na tamaa ya kulimbikiza mali na kupenda anasa. Kutokuwa na kiasi kumewapumbaza kiasi kwamba kila mmoja anafikiria namna ya kujinufaisha yeye mwenyewe kwanza.

Idadi ya vijana wanaokichukia Chama cha Mashetani nayo inazidi kuongezeka kila kukicha. Mawakala wa upandikazaji chuki hii ni umasikini, mfumko wa bei, ukiukwaji wa haki za binadamu, ubambikaji wa kesi dhidi ya watu unaofanywa na jeshi la polisi, matokeo mabaya ya mitihani ya taifa, huduma mbovu za kijamii na ubaguzi wa mikopo katika vyuo, ama kwa hakika, tunaangamia kwa kasi ya ajabu na matokeo ya siku za usoni yatakuwa mabaya zaidi kama hatutachukua hatua za haraka kulinusuru taifa kutoka kutoka katika utawala wa mashetani.

Leo hii ikitokea ajali hata ya baiskeli tu, ndani ya muda mfupi mamia ya vijana wanakusanyika kushangaa kuanzia asubuhi hadi jioni jua linapotua. Wanashangaa sio kwasababu wanapenda, la hasha, ni kwasababu hawana cha kufanya, wanaweza kushangaa hata wiki nzima. Hata wale wenye kujiajiri wanaishi maisha ya kubahatisha. Vijana wengi wanacheza bahati nasibu wakiwa na imani ya kufanikiwa siku moja kama wanavyohimizwa kupitia mitandao ya simu za mkononi, wanasema unalala, Unaamka Milionea. Hapa ndipo tulipofika baada ya safari ya miaka zaidi ya hamsini.

Taifa linashuhudia ongezeko la vitendo vya rushwa. Rushwa imekuwa ikidaiwa na kutolewa wakati wa kuwaandikisha watoto wa wanyonge shule. Walimu nao wamekuwa wakitoa rushwa ili waweze kupandishwa vyeo. Wagonjwa mahospitalini wanalazimika kutoa rushwa ili waweze kupatiwa dawa na vitanda ingawa huduma si za kuridhisha. Maofisa biashara nao wanadai rushwa ili kutoa leseni kwa mfanyabiashara ambaye hata mtaji wake wa biashara tu ni wa wasiwasi. Wanyonge hawana pa kukimbilia zaidi ya kulalamika kimoyomoyo. Pamoja na hayo yote, lakini ule mwisho umekaribia, mwisho wa kuangamizwa kwa chama cha mashetani.

photo


photo


photo


photo

Msanii Mkongwe wa Luninga na Vichekesho nchini Tanzania Asha Boko anategemea kuachia Video yake ya Kibonge Mnene mwisho wa mwezi huu. Video hiyo ambayo Audio yake ilifanyika katika Studio ya Kwanza Records iliyopo Morogoro imetayarishwa na Fasdo Video.Kwanza Records ni moja ya studio bora nchini Tanzania ambayo imekuwa ikisaidia kuinua vipaji vy muziki wa Bongo Fleva. Kwa wale wanaokumbuka Kwanza Records kwa mara ya Kwanza iliweza kumtambulisha Msanii Kitale aliyomshirikisha Marehemu Sharo Milionea iitwayo Hili Dude Noma.

Akiongea na Timu ya Mwaipaja Blog, Asha Boko amesema kuwa wadau wa Muziki wa Bongo Fleva wakae mkao wa kula kwakuwa amefanya mambo makubwa ndani ya Video hiyo.Asha Boko ametoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza kufanya naye kazi ikiwemo filamu, movie na Bongo Fleva.

Kwa watakaohitaji kuwasiliana na Asha Boko wawasiliane nae kwa namba yake ya mkononi ambayo ni 0754 273904 ila wasibip wala kumwomba Vocha

photo


Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya kumbukumbu  na Makamu wa Rais DktbMohamed Gharib Bilal pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Makatibu wakuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha  Mhe Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo (kuli) , anayekuwa balozi wa Tanzania nchini China. 
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha  Mhe Anthony Cheche (kushoto) anayekuwa Balozi wa Tanzania katika Congo DRC.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal wakiwa na mabalozi wapya walioapishwa leo Juni 11, 2013 katika Ikulu Ndogo Dodoma. Mabalozi hao ni Mhe Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo (kuli) , anayekuwa balozi wa Tanzania nchini China na Mhe Anthony Cheche (kushoto) anayekuwa Balozi wa Tanzania katika Congo DRC.
PICHA NA IKULU

photo ,


 Mrembo alieshikilia taji la Redd's Miss Arusha Glory Stephen  akipungia watu waliokuwemo katika kinyanganyiro hicho mara baada ya kutangazwa mshindi na nafasi ya pili ikiwa imeshikiliwa na Nance Mushi.
 Muaandaaji wa Redd's Miss kanda ya kaskazini Faustine Mwandago, akiwapongeza warembo walioshinda kinyanganyiro cha Arusha na kuwaahidi wote walioingia tano bora ,atawapa nafasi ya kushiriki katika kinyang'anyiro cha kumsaka mrembo wa kanda ya kaskazini.
Kulia ni mmoja wa waratibu wa shindano la REDD'S MISS ARUSHA 2013, Bi. Phide Mwakitalima pamoja na rafiki zake wakishuhudia mchuano wa warembo wa jiji la Arusha.
 mgeni Rasmi wa sherehe za kumsaka mlibwende wa Arusha (Redd's Miss Arusha)John  Mongela  katikati afisa utamaduni wa jiji la Arusha akifuatia wa kwanza  kulia ni muaandaaji wa Redd's Miss kanda ya kaskazini Mwandago. Picha kwa hisani ya Wazalendo 25 Blog

photo ,


 Msemaji wa Kamati ya Mazishi ya Marehemu Albert Mangwea ambaye pia ni Director kutoka Visual lab Bw Adam Juma akielezea ratiba ya Shughuli nzima ya Mazishi itakavyokuwa mara baada ya zoezi la kutoa heshima za mwisho zitakapomalizika
 Baadhi ya Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Wa Kwanza Kabisa ni Mkoloni akifuatiwa na Madee ambaye ni wa Tatu kutoka Mbele wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Marehemu Albert Mangwea
 Msanii Wa Muziki wa Kizazi Kipya Nasibu Abdul almaarufu kama Diamond akipita kutoa heshima zake za mwisho.
Baadhi ya Wasanii wa Fani mbalimbali pamoja na ndugu,jamaa na marafiki wakipita pembezoni mwa jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Albert Mangwea na kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu Albert Mangwea leo katika viwanja vya leaders
 Msanii wa Muziki Keisha (aliyejifunga kiremba Cheupe) akifuatiwa na Noora wakiwa na nyuso za huzuni wakati wakipita kwaajili ya kutoa heshima zao za mwisho katika viwanja vya leaders
 Wasanii wa fani ya Maigizo hapa Nchini Mzee Magari (aliyeshika Koti jeusi) akifuatiwa na Msanii Natasha Pamoja na Monalisa wakipita kwaajili ya Kutoa Heshima zao Za mwisho kwa Marehemu Albert Mangweha leo katika Viwanja vya leaders
Baadhi ya Ndugu, Jamaa na Marafiki wakitoa Heshima za Mwisho
Jeneza lenye Mwili wa Marehemu  Albert Mangweha likiwa juu ya meza tayari kwa Wakazi wa Jiji la Dar Kuanza kutoa Heshima Zao za Mwisho katika Viwanja Vya Leaders.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Habari, utamaduni na Michezo Bi Lilian Bereko akitoa Salamu za Rambirambi kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo leo katika viwanja vya leaders kabla ya Wakazi wa Jiji la Dar hawajaanza kutoa heshima zao za mwisho
Mmoja kati ya watu wa karibu wa Marehemu Albert Mangwea ambaye pia ni msanii wa muziki wa Kizazi kipya kutoka Katika Kundi aliloanzisha Marehemu Albert Mangwea Mez B akitoa historia fupi ya Kundi la Chamber Squade katika viwanja  vya leaders. Picha zote kwa hisani ya Lukaza Blog

photo ,