Jeneza liliobeba mwili wa marehemu.Marehemu Rajabu Tenga alikuwa pia mtumishi wa jeshi la polisi. (Usalama wa Raia). alifariki katika harakati za kuwaokoa wananchi na wanafunzi wenzake katika tukio la ujambazi lililohusisha kutupiana risasi kati ya majambazi na polisi.katika harakati hiyo ndipo jambazi moja lilipompiga risasi ya kichwa iliyopoteza maisha ya mwenzetu katika hospitali ya rufaa mbeya. (picha na Rayme A..K)
Wanafunzi wakiwa wamejipanga tayari kwa kuupokea mwili wa marehemu Tenga ...waliovaa jezi ni baadhi ya wachezaji wenzie wa mpira wa miguu enzi za uhai wake.
Gari la polisi lililobeba mwili wa marehemu likionekana kwa mbali likiingia katika viwanja vya chuo kikuu Mzumbe Mbeya - kampas
Mwili wa marehemu ukiingizwa chuoni na kikosi maalum cha ubebaji kilichoteuliwa kwa ajili ya kazi hiyo.
Wabebaji
Mwili ukishushwa na kuwekwa katika meza maalum
Tarehe 13/01/2007 Mzumbe brothers tukiwa katika kanisa la Mbeya Mjini tulipoalikwa kama kikundi katika tamasha lililofanyikia kanisani hapo
Wa kwanza kutoka kushoto ni Berius-anaimba sauti ya tatu
Marehemu Tenga wa pili kutoka kushoto-anaimba sauti ya nne
Mimi wa tatu niliyevaa batik na Magesa masige .
Hapa tuko katika ukumbi maarufu jijini Mbeya ujulikanao kama Dhandho tulipoalikwa kusindikiza uzinduzi wa kwaya ya kanisa la wasabato Mbeya Mjini.Mwenye suti ni mlezi wa chama cha wanafunzi wa kisabato Kampas ya Mbeya
Hapa marehemu Tenga akiwa na mchumba wake ambaye nae ni mwanafunzi wa chuo kikuu Mzumbe Mbeya Kampas......pole sana Dada Alavuya...mungu akupe uvumilivu. (Picha zote na Remigius A.K-Ambaye ndiye chif photographer wa blog hii)
Kwa mbali Turubai likionekana...wanafunzi wakiwa katika majonzi makubwa baada ya kupotelewa na mwanafunzi mwenzao...Rajabu Tenga aliyeuawa na majambazi jana jioni baada ya majambazi hayo kuvamia supamaket iliyoko karibu na chuo kikuu Mzumbe Mbeya campas.
WAOMBOLEZAJI
Belius na Mimi Tukiwa katika hali ya huzuni baada ya kupotelewa na mwimbaji mwenzetu (marehemu Tenga) tuliyekuwa tukiimba nae pamoja katika kundi la A cappella la Mzumbe Brothers.Marehemu Tenga alikuwa akiimba sauti ta nne (bez)
Huzuni ikiwa imetawala katika msiba...hapa wanafunzi wanasikiliza maelezo kutoka kwa mawaziri wa serikali ya wanafunzi (hawapo pichani)
Rajabu Tenga -mwanafunzi wa chuo kikuu Mzumbe kampas ya Mbeya ambaye amefariki jana jioni baada ya kupigwa risasi na majambazi waliovamia supa maket moja iliyoko jirani na chuo cha Mzumbe.
Taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kwenda nyumbani kwao Same zinafanyika.
Marehemu Tenga alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa pili- digrii ya sheria.
MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI................................
may be.....papot to be....msiandae malalamiko...kwa upande wangu nimeingia darasani mara kadhaa kufundisha...sijui kwa wenzangu...infact... all lekchalaz are equal.
Usinckeshe.....wakati mwingine mtu hulazimika kuangua kicheko pale pale point inapokuonekana.....Lintel akifurahi meno 30 na nje yote mbili katika mkutano wa wanafunzi ulioitishwa na co-ordinata na mkurugenzi msaidizi wa huku ughaibuni kwetu...Mbeya kampas
Hapa nimepozi na .......msije mkafikiri ndiye naniii...wangu
Ughaibuni kuzuri jamani...umeona kijani kibichi jinsi kilivyokubali hapo chini?
David Sechome-mwenye tshirt nyeupe akiwa katika mkutano uliofanyika jana ukijumuisha wanafunzi wote wa ughaibuni...
Mwanadada Lintel Komba ( anaetabasam)nae alikuwepo katika mkutano
Waziri mkuu wa uingereza Tony Blair (wa kwanza kushoto-mwenye tai nyekundu) akiwa amepozi na mmoja wa wananchi wake...imetoka eh?
Jamaa akionesha uhodari wake katika kile kinachoitwa...acrobatic................
Kuna kale katabia ka kuiga kila tunachokiona....tuige na hii
Hivi karibuni nikiwa katika safari yangu kuelekea ughaibuni....Mbeya Kampas..niliamua kushuka mji kasoro Bahari ili kusalimia ndugu na jamaa...hapa ni maeneo ya kilakala sekondari...kwa nyuma safu za milima ya uluguru zinaonekana live bila chenga.
Tatizo la kujiunganishia mipira ya maji halipo Dar peke yake...
Bahadhi ya barabara za mji kasoro bahari zinavyoonekana...muda mfupi tu ujao nitakuwa naelekea ughaibuni...tutakutana hukohuko
Mfalme mswati wa zwaziland akiwa katika pozi na mke wake wa kumi na mbili.
Mfalme mswati akiwa katika vazi la kiasili
Mama wa mfalme mswati
Mabiti wakielekea katika milima ya uswazi kwa ajili ya ngoma na sherehe ambapo mfalme hujitwalia mke kutoka miongoni mwa hawa unaowaona...sherehe hizi hufanyika kila mwaka kati ya mwezi agasti na disemba.
Mtoto wa mfalme mswati...ambaye hivi anasoma huko ughaibuni -uingereza..