Wanakijiji nikumbusheni...mnyama huyu huwakilisha nnini kwenye hela yetu?
Unaweza kupagundua mahali hapa? hivi watu wa mipango miji wanajua madhara ya kuruhusu ujenzi wa namna hii?ebu wadau wasilisheni hoja maana kila nikikumbuka kile kilichotokea katika soko la mwanjerwa moyo wangu huruka kichurachura
Hili ndilo kundi la Acappella kutoka Africa ya kusini lijulikanalo kama Ladysmith black Mambazo.Kundi hili linaimba muziki wa asili bila kutumia vyombo vya muziki yaani akapela na lilianzishwa mwaka 1964 na kiongozi wa kundi hilo - wa kwanza kutoka kushoto mstari wa mbele ambaye anaitwa Joseph shabalala.
Kundi hili ni moja ya vikundi maarufu duniani vinavyoimba muziki wa acappella kutoka Africa na kwa taarifa yako limesafiri na kushirikishwa na waimbaji mbalimbali maarufu duniani. Sauti za kundi hili ndizo zinazosikika katika ile picha ya Eddie Murphy iliyotokewa kupendwa sana ya COMING TO AMERICA.kama hujawahi kuitazama nenda kaikandamize sasa hivi.
Jamaa hawa wako mbioni kuja nchini Tanzania kwa udhamini wa Nyanza Company Limited
Hii imekaaje?
Mwanamke wa shoka...unamkumbuka huyu?.....hata kama humkumbuki lakini amini kuwa siku hazigandi
Hii ndiyo njia inayoelekea kituo cha watoto yatima Simike jijini Mbeya.......Kituo cha Simike kimeanzishwa miaka 17 iliyopita, wadau naomba niwapeleke moja kwa moja mkajionee wenyewe mandhari ya huko ili tusaidiane kwa pamoja katika kuwasaidia hawa wadogo zetu.
Safari yangu kuelekea kinjia hiko juu ilianzia hapa
Mtoto huyu umuoneaye hapo alipo hasikii, haoni na wala haongei.
Ni mmoja wa watoto yatima wanaolelewa na kituo cha Simike jiji Mbeya.
Wema Sepetu? !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Wadau toeni maoni juu ya hili......mimi naona haikubaliki totally
Ni vitu vya kawaida ukiwa ughaibuni kutinga makoti kama haya....nimepozi na Frank Zacharia..Mkurugenzi wa Nyanza Company Limited
Wabongo wengi wamekuwa na kasumba ya kuogopa kutoa damu...hivi tatizo ni nini?ukosefu wa elimu au?Michuzi unasemaje?kama huogopi njoo
Afande Sele akiwa katika pozi ndani ya gari lililokuwa likitumiwa na tour ya wanaume halisi na ndege tunduni...jamaa anatisha sana katika utunzi wa mashairi yaliyokwenda shule....Kitururu unamzungumziaje mshikaji huyu?...toa hoja
Ikulu inavyoonekana kwa mbele. Soma historia yake fupi hapa chini
Wadau wa Blog hii wakiwa katika nyuso za furaha.....kutoka kulia ni Teddy Sodoyeka, Neema Haki na rafiki yao kipenzi anayefanya makamuzi pale Hope Univeristy
Yale matokeo ya kidato cha sita yaliyokuwa yakisubiriwa kwa hamu kubwa na watahiniwa wa mtihani huo yameshatoka huku shule nyingi zikiwa zimefanya vibaya uklinganisha na miaka iliyopita. Kiwango cha kufaulu kwa mujibu wa baraza la mitihani la taifa kimepungua kwa asilimia sita ukilinganisha na mwaka jana.
Matokeo hayo hivi saa yanapatikana live bila chenga kupitia mtandao wa www.moe.go.tz
Bofya hapo kuangalia matokeo