Hili ndilo kundi la Acappella kutoka Africa ya kusini lijulikanalo kama Ladysmith black Mambazo.Kundi hili linaimba muziki wa asili bila kutumia vyombo vya muziki yaani akapela na lilianzishwa mwaka 1964 na kiongozi wa kundi hilo - wa kwanza kutoka kushoto mstari wa mbele ambaye anaitwa Joseph shabalala.
Kundi hili ni moja ya vikundi maarufu duniani vinavyoimba muziki wa acappella kutoka Africa na kwa taarifa yako limesafiri na kushirikishwa na waimbaji mbalimbali maarufu duniani. Sauti za kundi hili ndizo zinazosikika katika ile picha ya Eddie Murphy iliyotokewa kupendwa sana ya COMING TO AMERICA.kama hujawahi kuitazama nenda kaikandamize sasa hivi.
Jamaa hawa wako mbioni kuja nchini Tanzania kwa udhamini wa Nyanza Company Limited


1 Response so far.

  1. Hawa jamaa niliwacheki siku za karibuni.Kwa mpenda sanaa namshauri asiwamisi.Mambo zao baabu kubwa