Tumo katika taifa lililogubikwa na maswali. Watu hawaoni tena nuru kwa maisha yao ya baadae. Mazungumzo ya watu barabarani, kwenye vyombo vya usafiri, vyombo vya habari, maofisini, sehemu za ibada, vijiweni na kwenye mikusanyiko ya watu hujiuliza tunakwenda wapi. Ugumu wa maisha umewafanya wengine wazikimbie familia zao huku wengine kwa kuchanganyikiwa wamejiua na kuua familia zao.


Hali ya kukata tamaa iliyoenea miongoni mwa wananchi wengi haitokani tu na matatizo peke yake wala maovu katika jamii. Kinachokatisha tamaa zaidi ni kuona viongozi walioapa kuwalinda wanananchi dhidi ya uovu wakicheka na uovu wenyewe na wakati mwingine wanakumbatiana na waovu hadharani. Mpaka sasa hakuna dalili kwa viongozi kumaliza kucheka 


Serikali sasa inakabiliwa na changamoto nyingi kutoka kila upande. Ni kama mfumo mzima wa utawala umesimama na Mungu ndiye ajuaye nini kitatokea kesho na keshokutwa ndani ya taifa letu.  Nchi inakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira, umasikini uliokithiri, rushwa hususan kwenye mikataba ya kinyonyaji inayowanufaisha watu wachache katikati ya mamilioni ya watanzania. Uporaji wa rasilimali za taifa, mishahara midogo isiyoendana na hali ya maisha, kuporomoka kwa uchumi na huduma mbovu za kijamii ni baadhi tu ya dalili za ugonjwa hatari uliolikumba taifa.

(Hayo ni moja ya maelezo yaliyomo ndani ya kitabu changu cha shukrani ninachotarajia kukizinduwa mwishoni mwa mwezi wa tatu, kwa watakaohitaji nakala ya kitabu wasisite kunitafuta kupitia 0787 070707)

photo ,

0 Responses so far.