Kundi la Waimbaji wa Royal Advent Quartet wakiwajibika katika huduma ya Kiroho. Royal Advent ni moja ya makundi kongwe nchini Tanzania yanayoimba muziki wa Acappella (Muziki usiotumia vyombo vya Muziki). Kihistoria Muziki wa Acappella ni ni muziki wa kwanza kuimbwa duniani kabla ya ugunduzi wa vyombo vya muziki.
Mmoja kati ya waasisi na mwanaharakati aliyepigania kwa kuutangaza muziki wa Acappella nchini Tanzania ni Ndugu Amani Mwaipaja ambaye kwa jitihada za pekee alifanikiwa kusajili taasisi ya Acappella Kwanza ambayo inasimamia shughuli za muziki wa Acappella nchini Tanzania.
Katika historia ya Muziki wa Acappella nchini Tanzania, Tamasha la Kwanza la Muziki huo lilifanyika mwaka 2007 ndani ya Ukumbi wa Msimbazi Centre na kufanikiwa kuhudhuriwa na watu wengi ambao wengi wao walikuwa wakiusikia tu muziki huo kupitia radioni hasa Radio ya Morningstar ya Jijini DarEs Salaam..
Amani Mwaipaja mpaka sasa ni Mwenyekiti wa taasisi ya Acappella Kwanza ambayo mkao yako makuu yapo jijini Dar es Salaam. Moja ya Kikundi ambacho kimefanikiwa kujulikana sana miongoni mwa watanzania ni kundi la Acappella la The Voice ambalo lilijipatia umaarufu mkubwa kwa kutengeneza tangazo la mlio wa simu wa kampuni ya tigo
Mwaipaja Blog imefanikiwa kuongea na Mwenyekiti wa Acappella Kwanza Amani Mwaipaja ambaye ameiambia Mwaipaja Blog kuwa tamasha kubwa la Muziki wa Acappella linategemewa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Katika Picha hapo juu toka kushoto ni Mtangazaji Maduhu, Mbaraka Mchome,Yona
Japhet Msomi na Simon Mdee wakiimba kwenye mkutano wa makambi katika
Kanisa la Waadventista Wasabato Morogoro Mjini july 7,2007.