Mwanasheria Mshauri (Consultant) na Mwanaharakati wa Haki za Binadamu nchini Tanzania Ndugu Amani Mwaipaja anatarajiwa kuzindua Rasmi Huduma yake ya Ushauri wa Kisheria kwa nji ya Simu ifikapo katikati ya Mwezi Agosti Mwaka Huu.

Akizungumza na timu ya Mwaipaja Blog Mwanasheria huyo amesema kuwa lengo la huduma hiyo ni kuweza kuisaidia zaidi jamii iishiyo pembezoni na ambayo imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo kwa kutembea umbali mrefu ikitafuta msaada wa kisheria.
Kupitia huduma hiyo, watu mbalimbali watakaokabiliwa na matatizo ya kisheria wataweza kupata ushauri wa kisheria na kupewa mwongozo kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa kuuliza swali au kuomba ufafanuzi.

Akielezea upatikanaji wa huduma hiyo ya ushauri wa kisheria kwa njia ya simu mwaipaja alieleza taratibu za kujiunga kwa kuandika neno mwaipaja (Acha Nafsi) kisha andika ujumbe wako alafu utume kwenda namba 15678.

Mwaipaja alitoa wito kwa wote wenye kuhitaji huduma hiyo kujiunga na huduma hiyo kuanzia sasa kwakuwa tayari huduma hiyo imeshaanza kufanya kazi.

photo

0 Responses so far.