Mnamo tarehe 20/08/2013 majira ya 08.45 hrs. huko katika kijiji cha Fufu, Kata ya Fufu, Wilaya ya Chamwino, takribani magari matano (5) yaliyokuwa kwenye msafara wa Mwenge wa Uhuru, yakitokea Wilaya ya Dodoma kuelekea kwenye makabidhiano Wilaya ya Mpwapwa, moja ya magari yaliyokua kwenye msafara huo lilikutana na tuta huku dereva wake akishika ‘brake’ ghafla na kusababisha magari yaliyokuwa nyuma yake kugonga gari la mbele kwa kila moja lililokuwa likitimka kutokana na vumbi kubwa lililokuwa likifuka wakati wa msafara huo kufuatia matengenezo ya barabara Dodoma – Iringa yanayoendelea.

Katika ajali hiyo magari yaliyoathirika ni kama ifatavyo:-
1. STK 3007 TOYOTA LAND CRUISER
2. STK 3357 TOYOTA LAND CURISER yote ni mali ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa Katibu Tawala [M] Dodoma.
3. SM 5835 TOYOTA LAND CRUISER mali ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma
4. DFP.7178 TOYOTA LAND CRUISER (AMBULANCE) nayo ikiwa ni mali ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma.
5. T.627 BFJ TOYOTA LAND CRUISER mali ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma
6. STK 4983 TOYOTA LAND CRUISER HARD TOP Mali ya Wizara ya Kilimo. Watu wapatao tisa (9) walijeruhiwa katika ajali hiyo, kati yao wanne (4) wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa Dodoma na watano (5) walipatiwa matibabu na kuruhusuiwa kurudi nyumbani.

Majeruhi waliolazwa ni kama ifuatavyo:-
1. JUMA S/O ALLY @ SIMAI, Miaka 32, Mpemba, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Mkazi wa Kusini Unguja.
2. CHARLES S/O MAMBA, Mgogo, Miaka 50, Mkazi wa Ipagala, Diwani wa Kata ya Ipagala
3. DATIVA D/O KIMOLO, Miaka 46, Mrangi, Afisa Mifugo, Manispaa ya Dodoma, Mkazi wa Mailimbili.
4. AMINA D/O MGENI, Miaka 36, Muuguzi Kituo cha Afya Makole, Mkazi wa Area ‘C’ Manispaa ya Dodoma.

Majeruhi waliotibiwa na kuruhusiwa kurudi makwao ni kama ifuatavyo:-
1. JACKLINE D/O MAGOTI, Miaka 39, Mjita, Muuguzi Kituo cha Afya Makole, Mkazi wa Area C Manispaa ya Dodoma
2. RICHARD S/O MAHELELA, Miaka 51, Mgogo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Ipagala, Mkazi wa Ipagala Manispaa ya Dodoma
3. JUMANNE S/O NGEDE, Miaka 58, Mrangi, Diwani Kata ya Chamwino/ Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma, Mkazi wa Chamwino Manispaa ya Dodoma.
4. ZAITUNI D/O VARINOI, Miaka 43, Mkazi wa Mbwanga, Manispaa ya Dodoma.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linatoa wito kwa madereva na watumiaji wa barabara hususan zilizopo kwenye matengenezo wanapokuwa katika misafara, wanapaswa kuwa makini na wapeane nafasi kati ya gari moja hadi jingine ili kuepusha madhara yanayoweza kuepukika.

photo

0 Responses so far.