Dr Slaa akiwasili katika viwanja vya Kilombero Jijini Arusha

Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dr Wilbroad Slaa akizungumza na wananchi wa Jijini Arusha jioni ya leo katika muendelezo wa Mikutano ya wazi ya Mabaraza ya Kitaasisi ya Chadema kukusanya maoni ya Katiba Mpya kwa upande wa Chadema kama taasisi kamili.

Dr Slaa kwa siku ya leo amefanikiwa kufanya mikutano miine ya wazi Mkoani Arusha na baadae kushiriki katika kikao kingine cha mabaraza hayo cha ndani kilinachoendelea katika hoteli ya New Arusha.

Katika mikutano hiyo Dr Slaa ameambatana na wanasheria wa chama akiwemo Mabere Marando pamoja na viongozi wengine kutoka makao makuu akiwemo mjumbe wa Kamati Kuu Dr Kitila Mkumbo.

Wananchi mbali mbali walipata fursa ya kutoa maoni yao hadharani katika mjumuiko huo uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi, na kujaza eneo la wazi katika viwanja vya Kilombero Jijini hapa.

Chadema wamepanga kuzunguka nchi nzima kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya ya Tanzania wakiwa na lengo la kukusanya maoni ya watu wasiopungua milioni 8. Tayari viongozi mbalimbali wa chama hicho wametawanyika maeneo tofauti ya nchi kuendesha vikao vya mabaraza hayo.

Awali wanasheria mbalimbali wa chama Mkoa wa Arusha walikuwa wakiwaelimisha wananchi masuala mbali mbali kuhusiana na Katiba na sheria kwa ujumla katika kuwaanda vyema kabla ya kutoa maoni yao.


Mratibu wa vikao vya mabaraza ya Chadema, mh Mwita Waitara akisalimia wananchi kabla ya kumkaribisha Wakili Mabere Marando ambye pia alimkaribisha Dk Slaa


Mwanasheria wa Chadema na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama, Wakili Mabere Marando akichambua baadhi ya vifungu vya rasimu ya Katiba inayokusudiwa kutolewa maoni na wananchi. Marando amesema kwa upande wa Chadema wanaunga mkono zaidi ya asilimia 80 ya mambo yaliyomo katika rasimu hiyo iliyoandaliwa na Tume inayoongozwa na jaji Warioba.


Wananchi wakifuatilia kwa makini maoni mbalimbali


Baadhi ya wananchi wakinyoosha mikono kuashiria kukubaliana na maoni ya mwenzao aliyependekeza vyeo vya ukuu wa wilaya na mkoa kuondolewa kabisa kwenye katiba mpya na badala yake viongozi wa ngazi hizo wachaguliwe na wananchi wa maeneo husika. Zoezi hilo la kutoa maoni lilikuwa linasimamiwa na Dk Slaa


Wanasheria vijana wakiwafafanulia wananchi vipengele mbalimbali vya rasimu ya Katiba. Mwenye suti ni James Lyatuu na mwenye tisheti ya mistari ni Mathias Lyamunda


Kulikuwa na fomu nyingi zilizogawiwa kwa wananchi wengine kutoa maoni yao kwa kuandika kama huyu

Wakili Marando akisoma habari kwenye gazeti

Dk Slaa akibadilishana taarifa na viongozi wa Mkoa wa Arusha na Kanda ya Kaskazini, wakati huo huo Marando akizungumza na Ally Bananga. KWA MENGI ZAIDI BOFYA HAPA >>>

photo ,

0 Responses so far.