Ni Koplo Ernest, Yusuph, Jackson, Juliana Tadei na Mohamed.
 Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe amewafukuza kazi na kuliagiza jeshi la Polisi nchini kuwaunganisha na wengine kwenye kesi mahakamani ili kujibu mashitaka ya jinai, wale wote waliohusika katika kuuwasaidia Agnes Gerald na mwenzake Mellisa kupitisha dawa za kulevya kuelekea Afrika Kusini ambako walikamatwa katika kiwanja cha Ndege cha Oliver Thambo nchini humo.

Waziri Mwakyembe ametoa agizo hilo leo, ofisini kwake, mbele ya waandishi wa habari wakati alipowaita ili kuufahamisha umma kuhusu hatua zilizochukuliwa na Wizaa yake kuhusu suala la dawa za kulevya

Aidha, amesema wafukuzwe mara moja ni baada ya kupitia CCTV na kuona namna walivyohusika siku hiyo kwani walionekana wakipiga simu mara watoke nje kinyume na sheria za chumba cha ukaguzi (vifaa hivi ni kama vilivyotumika na CHADEMA kuwanasa polisi waliorusha bomu na baadae kuwashambulia kwa risasi).
Hao waliotajwa hapo juu ni waliofanikisha kupitisha kilo 180 zilizokuwa zimebebwa na wasichana wawili (Masogange na mwenzake) waliokamatwa huko Afrika kusini.

photo

0 Responses so far.