Wanakijiji nikumbusheni...mnyama huyu huwakilisha nnini kwenye hela yetu?
Unaweza kupagundua mahali hapa? hivi watu wa mipango miji wanajua madhara ya kuruhusu ujenzi wa namna hii?ebu wadau wasilisheni hoja maana kila nikikumbuka kile kilichotokea katika soko la mwanjerwa moyo wangu huruka kichurachura
Hili ndilo kundi la Acappella kutoka Africa ya kusini lijulikanalo kama Ladysmith black Mambazo.Kundi hili linaimba muziki wa asili bila kutumia vyombo vya muziki yaani akapela na lilianzishwa mwaka 1964 na kiongozi wa kundi hilo - wa kwanza kutoka kushoto mstari wa mbele ambaye anaitwa Joseph shabalala.
Kundi hili ni moja ya vikundi maarufu duniani vinavyoimba muziki wa acappella kutoka Africa na kwa taarifa yako limesafiri na kushirikishwa na waimbaji mbalimbali maarufu duniani. Sauti za kundi hili ndizo zinazosikika katika ile picha ya Eddie Murphy iliyotokewa kupendwa sana ya COMING TO AMERICA.kama hujawahi kuitazama nenda kaikandamize sasa hivi.
Jamaa hawa wako mbioni kuja nchini Tanzania kwa udhamini wa Nyanza Company Limited
Hii imekaaje?
Mwanamke wa shoka...unamkumbuka huyu?.....hata kama humkumbuki lakini amini kuwa siku hazigandi
Hii ndiyo njia inayoelekea kituo cha watoto yatima Simike jijini Mbeya.......Kituo cha Simike kimeanzishwa miaka 17 iliyopita, wadau naomba niwapeleke moja kwa moja mkajionee wenyewe mandhari ya huko ili tusaidiane kwa pamoja katika kuwasaidia hawa wadogo zetu.
Safari yangu kuelekea kinjia hiko juu ilianzia hapa
Mtoto huyu umuoneaye hapo alipo hasikii, haoni na wala haongei.
Ni mmoja wa watoto yatima wanaolelewa na kituo cha Simike jiji Mbeya.
Wema Sepetu? !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Wadau toeni maoni juu ya hili......mimi naona haikubaliki totally
Ni vitu vya kawaida ukiwa ughaibuni kutinga makoti kama haya....nimepozi na Frank Zacharia..Mkurugenzi wa Nyanza Company Limited
Wabongo wengi wamekuwa na kasumba ya kuogopa kutoa damu...hivi tatizo ni nini?ukosefu wa elimu au?Michuzi unasemaje?kama huogopi njoo
Afande Sele akiwa katika pozi ndani ya gari lililokuwa likitumiwa na tour ya wanaume halisi na ndege tunduni...jamaa anatisha sana katika utunzi wa mashairi yaliyokwenda shule....Kitururu unamzungumziaje mshikaji huyu?...toa hoja
Ikulu inavyoonekana kwa mbele. Soma historia yake fupi hapa chini
Wadau wa Blog hii wakiwa katika nyuso za furaha.....kutoka kulia ni Teddy Sodoyeka, Neema Haki na rafiki yao kipenzi anayefanya makamuzi pale Hope Univeristy
Yale matokeo ya kidato cha sita yaliyokuwa yakisubiriwa kwa hamu kubwa na watahiniwa wa mtihani huo yameshatoka huku shule nyingi zikiwa zimefanya vibaya uklinganisha na miaka iliyopita. Kiwango cha kufaulu kwa mujibu wa baraza la mitihani la taifa kimepungua kwa asilimia sita ukilinganisha na mwaka jana.
Matokeo hayo hivi saa yanapatikana live bila chenga kupitia mtandao wa www.moe.go.tz
Bofya hapo kuangalia matokeo
Huyu ndiye Miss Tanzania wa kwanza kabisa ambaye kaka michuzi ametupatia taarifa za hivi karibuni kuwa hatuko naye tena duniani....alikuwa akijulikana kwa jina la mama theresa. kwa habari zaidi bofya hapa
Hawa ni moja kati ya watoto wengi waliotoka kufanyiwa.....kwa habari zaidi bofya hapa www.saharanvibe
Hili ni ziwa masoko..ni moja kati ya maziwa machache yenye maajabu na historia ya pekee kama ile ya Ziwa kisiba....watu mbalimbali hufika kuangalia mandhari ya ziwa hili lililozungukwa na milima.
Mashamba ya chai
Mlima Rungwe unavyoonekana kwa mbali
Wanajiografia nisaidieni....hii inaitwa nini vile?
Hili ndilo daraja laMungu lililoko mbele kidogo ya Kiwira.Hapo zamani daraja hili lilikuwa na maajabu ya pekee.Siwezi kueleza maajabu yote lakini hiko kidaraja unachokiona hapo hakijawahi kujaa hata siku moja hata mafuriko yawe makubwa kiasi gani...
Haya ndiyo maporomoko ya Kaporogwe...kwa kidhungu wanasema ..Kaporogwe falls
Mto Kiwira
Hivi karibuni nimepata maoni kupitia email na namba yangu ya simu kutoka kwa wadau mbalimbali wa blog hii kuwa wanapata shida sana katika taratibu za kutuma maoni yao.
Zifuatazo ni hatua muhimu katika kutuma maoni kupitia blog hii
1. Bofya kwenye sehemu iliyoandikwa maoni
2. ikishafunguka bofya tena sehemu iliyoandikwa post a comment
3.Ikifunguka anza kuandika maoni yako
4.Jaza maneno yanayoonekana katika kiboksi (word verification) kisha
5.Chagua sehemu iliyoandikwa anonymous kisha
6.Bofya sehemu iliyoandikwa "publish your comment "
Ukikamilisha taratibu hizi hapo maoni yako yatachapishwa moja kwa moja katika sehemu ya maoni.
Karibu tena....